25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAWAZIRI WALIVYOWAAGA MARIA, CONSOLATHA

Mwandishi Wetu, Iringa

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu), Ikupa Alex wamewaelezea  Maria na Consolatha kuwa walikuwa watu wenye upendo na uvumulivu huku wakisisitiza watu wengine kuishi maisha ya aina hiyo.

Kauli hizo wamezitoa kwa nyakati tofauti wakati wa kuagwa kwa mapacha hao walioungana  waliofariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili wiki hii katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa, wanaotarajiwa kuzikwa leo.

Profesa Ndalichako na Naibu Waziri Ikupa, ni miongoni mwa viongozi wa serikali waliohudhuria misa ya kuwaaga marehemu Maria na Consolata na iliyofanyika mkoani Iringa na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa.

“Kuishi kwa hali kama hiyo kwa umri 21 ni suala linaloweza kuwafundisha Watanzania uvumilivu lakini pia tutawakumbuka kwa umoja wao katika shida na raha, tunatakiwa tuige mfano tupendane na tushirikiane tujifunze kupitia hili” amesema Profesa Ndalichako.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ikupa, amesema pamoja na hali waliyokuwa nayo, bado waliona hakuna kitakachoweza kuwatenganisha na Mungu.

“Wao hata ulemavu usingeweza kuwatenga na Mungu wao, kikubwa tunaweza kujifunza kwa hawa watoto ni kutokata tamaa katika maisha kwa hali yoyote,” amesema .

Maria na Consolata wanazikwa leo kijijini Ipamba Wilaya ya Iringa katika makaburi ya viongozi wa Kanisa Katoliki, Tosamaganga.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles