30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

SERIKALI YAWATIKISA MAASKOFU WA KKKT

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM


SERIKALI imeliandikia barua Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ikilitaka kuufuta waraka wa Pasaka uliotolewa Machi mwaka huu vinginevyo hatua kali za sheria zitachukuliwa dhidi ya kanisa hilo.

Waraka huo uliopewa jina la ‘Taifa letu amani yetu’ ulisainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo. Ulijikita kujadili masuala ya jamii, uchumi, siasa, katiba mpya na matukio ambayo yako kinyume na kile lilichokiita tunu na misingi ya Taifa.

Jana, Mtanzania ilimtafuta Kiongozi wa Kanisa hilo, Askofu Dk. William Shoo kwa njia ya simu kuzungumzia

barua hiyo ya serikali lakini hakupatikana.

Pia Mtanzania lilifi ka ofi si za makao makuu ya KKKT mjini Arusha kuonana na katibu mkuu wa kanisa hilo ambaye hakuweza kupatikana.

Katibu muhtasi wake alisema kiongozi huyo alikuwa nje ya ofisi akihudhuria vikao nje ya ofisi.

Mwandishi aliacha mawasiliano yake ofi sini hapo baada ya kushauriwa kuacha namba yake ya simu ili apigiwe

baadaye baada ya kiongozi huyo kutoka kwenye vikao.

Hata hivyo hadi gazeti linakwenda mtamboni jana usiku hakuna simu yoyote iliyopigwa kwa mwandishi kutoka

makao makuu ya kanisa hilo.

Alipotafutwa, mmoja wa maaskofu waliosaini waraka huo ambaye ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,

Dk. Stephen Munga, alisema hajapata taarifa yoyote kama kuna barua yoyote kutoka serikalini ikizungumzia waraka huo.

“Jana usiku nilipigiwa simu na mtu mmoja akiniuliza jambo hilo na nimebaki mdomo wazi mpaka sasa kwa sababu sijapata ‘offi cial communiqué’ kutoka kwa askofu yeyote.

“Nimeona kwenye mitandao lakini mitandao ina mambo mengi…sipendi kuamini kwamba serikali inaweza kutoa

kauli ya hivyo kwa hiyo tusubiri,” alisema Askofu Munga.

Agizo la Serikali Msajili wa Vyama katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, L. Komba, kupitia barua ya Mei 30 yenye kumbukumbu namba SO. 748/25, alitoa agizo hilo kwa KKKT ikiwa ni zaidi ya miezi miwili tangu utolewe waraka huo wa maaskofu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, kanisa hilo limetakiwa kuufuta waraka huo ndani ya siku 10 tangu kupokewa barua hiyo vinginevyo hatua kali za sheria zitachukuliwa.

“Ofi si ya Msajili imejiridhisha kuwa taasisi unayoiongoza imeunda chombo kisicho cha sheria kinachoitwa Baraza

la Maaskofu la Kanisa la KKKT na mmetoa waraka mliouweka majina ya maaskofu na kuusambaza kwa umma wa Tanzania kinyume cha sheria.

“Waraka huo unaonyesha dhahiri haukuwa na lengo zuri kwa vile umehusisha taasisi yenu na masuala ambayo

yapo nje ya imani.

“Ni wazi kwamba mlikuwa na nafasi ya kuishauri mamlaka ya nchi au kuzishauri mamlaka mbalimbali za serikali kuhusu kile mlichokiona ndani ya jamii, kama kipo, badala ya kutoa maandishi kwa umma ambayo ofi si ya msajili inaona yanaweza kuamsha hisia na kuleta tafsiri mbalimbali zenye mitazamo tofauti na muelekeo mbaya kwa jamii nataifa kwa ujumla.

“Kwa vile kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheriaya Vyama Sura 337 na kwa vile ‘baraza’

hilo halitambuliki kisheria katika ofi si ya msajili, unaelekezwa kuufuta waraka husika kwa maandishi na kuujulisha umma kuwa taasisi yako haikuwa na haina uwezo katika sheria kufanya kile mlichokifanya.

 

“Maandishi hayo yaufi kie umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari na njia nyingine zilizotumika kuufi kasha waraka ule,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

Serikali pia ililiandikia kanisa hilo barua nyingine, Mei 10 na Mei 22 mwaka huu.

Vilevile kimekwisha kufanyika kikao baina ya kanisa hilo na ofi si ya msajili, Mei 29 mwaka huu.

Hata hivyo Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Shoo anadaiwa hakuhudhuria kikao hicho na hivyo akatakiwa afi ke ofi sini kwa msajili.

 

“Wewe askofu kiongozi wa taasisi hii umeshindwa kutii wito wa kufi ka ofi si ya msajili kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 33 cha Sheria ya Jumuiya sura ya 337. Kufanya hivyo ni kosa la jinai na unahitajika kufi ka mbele ya msajili wa vyama,” ilieleza sehemu nyingine ya barua hiyo.

Barua hiyo pia imelitaka kanisa hilo kulipa madeni yote ya ada kwa serikali ndani ya siku saba pamoja na kuijulisha ofisi ya msajili mabadiliko ya uongozi uliowahi kufanywa katika kanisa hilo.

“Taasisi unayoiongoza imethibitika kutotekeleza masharti ya usajili kwa kushindwa kulipa ada za mwaka, kutoa

taarifa za mikutano, taarifa za fedha na mabadiliko mbalimbali, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

“Katiba inayotambulika kutumiwa kuongoza taasisi ni ile iliyoandaliwa mwaka 1960 na kupitishwa na kukubaliwa na ofi si ya msajili mwaka 1963.

“Mnapaswa kuomba ridhaa ya ofi si ya msajili ya kurekebisha katiba kwa kujaza fomu husika ili mkikubaliwa muweze kupewa maelekezo ya kufuata kurekebisha katiba yenu,” ilieleza barua hiyo.

Jana, Mtanzania ilifi ka kwenye ofi si za Wizara ya Mambo ya Ndani na kukutana na ofi sa mmoja ambaye hakutaka kunukuliwa, ambaye alikiri kuwa taarifa hiyo ni ya msajili wa vyama vya raia. 

WARAKA ULIVYOKUWA

Maaskofu 27 wa KKKT walikutana Machi 15 mwaka huu na kutoa waraka huo uliopangwa kusomwa katika makanisa yote ya kanisa hilo wakati wa Sikukuu ya Pasaka.

Hata hivyo wakati wa Sikukuu ya Pasaka baadhi ya makanisa yakiwamo ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani hayakuusoma waraka huo.

Siku chache baadaye, Baraza la Maaskofu wa Kanisa hilo lilimtenga Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, kwa kwa kile kilichoelezwa kuwa alizuia waraka huo kusomwa katika dayosisi anayoiongoza.

Uamuzi huo ulifi kiwa baada ya kikao cha maaskofu 25 waliokutana Aprili 24 na 25 Arusha kikao kilichoongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Fredrick Shoo.

Kikao hicho kiliwapa muda maaskofu hao hadi Septemba mwaka huu wawe wameliomba radhi kanisa na kuandika barua ya kueleza kama wanaukubali au kuukataa waraka huo.

Mbali ya Dk. Malasusa, maaskofu wengine ni Lucas Mbedule (Dayosisi ya Kusini Mashariki) na Dk. Solomon Massangwa (Dayosisi ya Kaskazini Kati).

Askofu Mbedule aliwaomba radhi waumini wa kanisa hilo wakati wa ibada iliyofanyika Aprili 29 katika Kanisa Kuu

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles