23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAPEWA SIKU SABA KUWAOMBA RADHI WALEMAVU

Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu, Abubakar, Akeshi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kupinga vitendo vya unyanyasaji walivyofanyiwa na Jeshi la Polisi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Anna Henga na Mkurugenzi mtendaji wa haki za watu wenye ulemavu, David Nyendo. Picha na Jumanne Juma

Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa siku saba kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwaomba msamaha walemavu kwa udhalilishaji waliowafawanyia.

Pia wamelitaka jeshi hilo kulipa fidia ya baiskeli za walemavu 30, zilizoharibiwa kutokana na shambulizi la polisi pamoja na simu za mkononi na fedha.

Wamesema wasipofanya hivyo, watachukua hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani.

Juni 16 mwaka huu, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liliwaadhibu watu wenye ulemavu waliokuwa wakifanya maandamano ya kupinga kuzuiwa kuingia katikati ya jiji wakiwa na bajaji zao.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga alisema siku hiyo polisi walitumia nguvu iliyopitiliza na kinyume cha utaratibu kwa kufanya manyanyaso yaliyopitiliza kwa walemavu wanawake ambao walifunuliwa nguo zao na askari wa kiume.

“Jambo hili ni fedheha , udhalilishaji na linatweza utu wa mwanamke na kitendo hiki si cha kiungwana na tunakikemea vikali,”alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa Watu Wenye Ulemavu, David Nyendo alisema walemavu hawakufanya maandamano bali ni madereva wa bajaji walikwenda kumwona Mkurugenzi wa Manispaa wapewe sehemu maalumu ya kupaki bajaji zao.

“Ndani ya siku saba, Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi hilo, kwa namna yoyote ile litakavyoona vema lijitokeze hadharani kuwaomba msamaha watu wenye ulamavu na taifa kwa ujumla kwa kitendo cha udhalilishaji kilichotekelezwa na maafisa wake.

“Kinyume na hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Jeshi la Polisi.

“Pia ndani ya muda huo hu, tunaliomba jeshi hilo litoe fidia ama nafuu kwa waathirika wa shambulizi hilo ambazo ni; baiskeli za walemavu 30 ambazo ziliharibika kutokana na shambulizi la polisi,”alisema Nyendo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles