24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

‘MCHAKATO WALIOBEBA MIMBA KURUDI SHULE UHARAKISHWE’

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi HakiElimu, John Kalage

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

TAASISI ya HakiElimu imeitaka Serikali kuharakisha upitiaji na upitishwaji wa miongozo ili watoto wa kike waliojifungua warejee shuleni na kuendelea na masomo.

Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, John Kalage, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha ufanikishaji wa elimu ya mtoto wa kike.

Alisema mwaka 2015 pekee, watoto wa kike takribani 3,690 wa shule za msingi na sekondari  nchini walipata ujauzito na kufukuzwa shule na hivyo kukatisha ndoto zao za mafanikio ya kupata elimu katika maisha.

“Kwa kuwa elimu ni haki ya msingi kwa kila mtanzania, Serikali haina budi kuharakisha upitiaji na upitishwaji wa miongozo ili watoto hao waweze kuendelea na masomo haraka iwezekanavyo ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Kuwarejesha watoto wa kike waliopata mimba inatokana na ukweli kuwa baadhi ya watoto wa kike hupata mimba kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao ikiwemo kubakwa au kudanganywa kutokana na shida wanazokumbana nazo katika mfumo wa elimu, hivyo ni lazima  tuelewe kuwa changamoto nyingi zinazosababisha pia zinatokana na changamoto ya mfumo wa elimu pia,’’alisema Kalage.

Kalage pia alielezea hali halisi ya mtoto wa kike ikiwemo sababu zinazowafanya watoto wengi kuacha shule kila mwaka huku akitolea mfano mwaka 2015 watoto wa kike 69,067 wa shule za  sekondari waliacha shule kwa sababu ya mimba, utoro na vifo.

Sababu nyingine ni hali ya uandikishaji na upatikanaji wa fursa za kuwa shuleni, mazingira ya kujifunzia na kufundishia, kutoshughulikiwa kwa changamoto za kimaumbile, unyanyasaji wa kijinsia.

Pia ukosefu wa mabweni na changamoto za umbali alisema unasababishwa na changamoto za usafiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles