23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WENYE URAIA WA NCHI MBILI KUNY’ANG’ANYWA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

NA KULWA MZEE-DODOMA

SERIKALI imetangaza kuwanyang’anya  umiliki wa ardhi watu wenye uraia wa nchi mbili na imeondoa tozo kubwa ya asilimia 67 iliyokuwa ikiwakwaza Watanzania na wawekezaji katika umiliki wa ardhi.

Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alipokuwa akichangia na kujibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge,

Lukuvi alisema baada ya kuondoa tozo hiyo, kodi mpya itaanza kutumika Julai mwaka huu. Kwamba kama kuna mtu alikuwa anatakiwa kulipa Sh milioni 100 sasa atalipa Sh milioni 33, lengo likiwa ni kuwapa nafuu Watanzania wote waweze kumiliki ardhi na Serikali kupata mapato.

Alisema wawekezaji walikuwa hawawezi kufika Dodoma kwa sababu ya mkanganyiko wa umilikaji wa ardhi.

“Sasa hivi wenye hati za kumilii ardhi kwa miaka 33 wataendelea kupata hati za miaka 99 kama ilivyo kwa watu wengine nchini,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles