25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm: Naheshimu maamuzi ya kutimuliwa Niyonzima

PLUJMADAM MKWEPU NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga, Hans van der Pluijm, amesema anaheshimu uamuzi uliotolewa na uongozi wa klabu hiyo juu ya kuvunja mkataba wa aliyekuwa kiungo mkabaji wa timu hiyo, Haruna Niyonzima.

Uongozi wa Yanga ulifika tamati na mchezaji huyo juzi, kwa madai ya kuchoshwa na tabia yake ya kutoheshimu mkataba pamoja na kutaka kuwa juu ya klabu.

Niyonzima aliongezewa mkataba wa miaka miwili Mei 19 mwaka huu, lakini kutokana na hatua hiyo alitakiwa kulipa gharama ya mkataba huo dola za Kimarekani 71,175 ambayo ni sawa na fedha za Tanzania Sh milioni 152.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam, baada ya kumaliza mazoezi yaliyokuwa yakifanyika katika Uwanja wa Boko Veteran, Pluijm alisema hatoweza kuzungumzia jambo ambalo tayari limefanyiwa uamuzi na uongozi.

“Namfahamu Niyonzima alikuwa mchezaji wangu lakini tayari uongozi umeshaamua siwezi kuujadili uamuzi huo kwa kuwa nauheshimu,” alisema Pluijm.

Akizungumzia michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kutimua vumbi Januari 2 mwakani katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, alisema haofii timu yoyote katika kundi alilopangwa kwenye michuano hiyo.

Katika michuano hiyo, Yanga imepangwa kundi B, ikiwa na Azam FC, Mafunzo pamoja na Mtibwa Sugar ya Ligi Kuu Bara.

“Tupo na Azam naijua pia wanatujua, hivyo mchezo dhidi yao utakuwa mgumu hata kwa timu nyingine, lakini sitakuwa tayari kuachia pointi kwa timu yoyote ile kwa kuwa lengo letu ni kunyakuwa ubingwa kwani nimewaandaa wachezaji wangu kupata ushindi katika kila mechi,” alisema Pluijm.

Aidha, kocha huyo alisema kwamba  mchezo wao dhidi ya Mafunzo watakaocheza Jumapili hii utakuwa  mgumu na kudai kwamba hakuna timu ya kubeza kwa sababu zote zipo vizuri.

Yanga inatarajia kuelekea Zanzibar kesho kuanza michuano hiyo ambapo Jumapili ya wiki hii watacheza na timu ya Mafunzo, huku Azam wakikutana na Mtibwa Sugar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles