24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Ulimwengu kutua Besiktas Uturuki

Thomas+Ulimwengu+Club+America+v+TP+Mazembe+E5RcS2Rbf4flNA MWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa Taifa Stars na klabu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu yupo njiani kujiunga na klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki.

Taarifa hii inakuja ikiwa ni siku chache tangu nyota mwingine wa Tanzania anayekipiga naye katika klabu ya Mazembe, Mbwana Samatta, kuwa kwenye mazungumzo na klabu ya K.R.C Genk ya nchini Ubelgiji

Chanzo cha karibu na Ulimwengu kimesema kuwa tayari Besiktas wameanza mazungumzo ya awali na mchezaji huyo aliyetokea kwenye Akademi ya Shirikisho la Soka nchini, TFF.

Lakini pamoja na mazungumzo hayo, Ulimwengu itabidi asubiri hadi Februari mwakani, ili aweze kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo mwishoni mwa msimu na hii ni kwa sababu Mazembe wameweka ngumu kumuuza.

Mkataba wa Ulimwengu na Mazembe unamalizika Agosti mwakani, lakini kwa kipindi kirefu straika huyu alikuwa akipambana na uongozi wa Mazembe umuuze lakini zoezi hilo likawa gumu.

Kama atafanikiwa kujiunga na Besiktas inayoongoza msimamo wa ligi kuu nchini Uturuki, wakijikusanyia pointi 41 baada ya michezo 17 waliyocheza mpaka sasa, Ulimwengu atapata nafasi ya kucheza pamoja na wachezaji nyota duniani akiwemo winga wa kimataifa wa Ureno, Ricardo Quaresma, aliyewahi kutamba katika klabu za Barcelona, Inter Milan na Chelsea.

Besiktas iliyoanzishwa Machi 1903, wametwaa ubingwa wa ligi Uturuki mara 13 huku wakiwa na rekodi ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1987 na robo fainali ya Kombe la Europa mwaka 2003.

Kwa mujibu wa viwango vya Uefa vinavyoonyesha ubora wa klabu barani Ulaya, Besiktas wanashika nafasi ya 61 huku Genk ya Samatta inakamata nafasi ya 59.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles