Weusi kufunga mwaka Arusha

0
1582

WeusiNA CHRISTOPHER MSEKENA

KUNDI la muziki wa hip hop nchini, Weusi linatarajia kufunga mwaka na kuufungua mwaka mpya nyumbani kwao Arusha katika viwanja tofauti tofauti.

Akizungumza na MTANZANIA moja ya wasanii wanaounda kundi hilo, Nikki wa Pili alisema kuwa wameamua kufunga mwaka nyumbani kwao kwa sababu mwaka mzima walikuwa wakifanya maonyesho maeneo mengine ya Tanzania.

“Tunarudi nyumbani kutoa burudani kwa mashabiki wetu, kwa mwaka mzima tumekuwa tukifanya maonyesho maeneo mbalimbali lakini Weusi hatukuwahi kutumbuiza Arusha kwa hiyo hii ni nafasi nzuri kwa wapenzi wote wa Nikki, G Nako na Joh Makini kufurahia muziki mzuri,” alisema Nikki wa Pili.

Aliongeza kuwa mbali na Weusi, Vanessa Mdee naye atajumuika nao kutoa burudani kwenye Uwanja wa Triple A na mwaka mpya watakuwepo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuwaburudisha mashabiki wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here