24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NHIF yajipanga kuwafikia wananchi

Elizebth kilindi – Njombe

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Njombe, Abdiel Mkaro amesema wamejipanga kufikia asilimia 50 ya wananchi mkoani humo kusajiliwa kwenye bima ya afya ili kuweza kupata huduma za uhakika pindi wanapougua.

Hayo aliyasema jana alipokuwa akizungumza na MTANZANIA.

Mkaro alisema kuwa ili kuweza kufikia lengo, mfuko wa bima ya afya taifa ulizindua vifurushi ambavyo vinawezesha kila Mtanzania aweze kujipimia kulingana na uhitaji wake, uwezo wake na ukubwa wa familia yake.

“Katika hivi vifurushi tumejipanga kuendana na umri, tumeanza na umri wa miaka 18 mpaka miaka 35, hilo ni kundi la kwanza, kundi la pili miaka 36 mpaka 59 na kundi la tatu ni miaka 60 na kuendelea, kwa hiyo kadiri umri unavyokuwa mkubwa basi kiwango cha kuchangia kinakuwa kikubwa.

“Na hivi vifurushi tumeviweka kwa makundi; cha mtu mmoja, wanandoa, wanandoa na mtoto mmoja, wanandoa na watoto wawili, wanandoa na watoto watatu, wanandoa na watoto wanne. Pia kuna ya mzazi mtoto mmoja wale ambao hawana ndoa, mzazi watoto wawili, mzazi watoto watatu na mzazi watoto wanne,” alisema Mkaro.

Aidha alisema Mkoa wa Njombe wamejipanga kufikia watu popote walipo kama vile stendi za mabasi, masokoni pamoja na kutumia magari ya matangazo kupita kwenye mitaa, nyumba za ibada kutoa elimu kuhusu vifurushi vipya vilivyozinduliwa.

“Pia tutawafikia viongozi wa Serikali kuwapa elimu ili wakatusemehe au tuambatane nao wanapokuwa kwenye ziara za kutembelea wananchi ili na sisi tuweze kutoa elimu hii kwa wananchi kwa sababu bado uelewa ni mdogo,’’ alisema Mkaro.

Pamoja na hayo, Mkaro alisema bado wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya watoa huduma ambao si waaminifu ambao wanafanya udanganyifu katika madai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles