24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanajeshi Urusi awapiga wenzake wanane risasi

MOSCOW-Urusi

MWANAJESHI mmoja wa Urusi amewapiga risasi wanajeshi wenzake wanane na kuwajeruhi vibaya wengine wawili katika kambi ya kijeshi iliopo mashariki kulingana na maofisa.

Askari huyo, Ramil Shamsutdinov ambaye alikamatwa huenda alikuwa akiugua tatizo la kiakili.

Tukio hilo lilifanyika katika kitengo cha kijeshi nambari 54160 katika kijiji cha Gorny sio mbali na mji wa Chita Ijumaa jioni.

Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa 12:15 kulingana na kamati ya uchunguzi ya Urusi.

Wizara ya Ulinzi  ilisema risasi zilifyatuliwa wakati wa kubadilishana zamu katika eneo la Transbaikal.

Shamsutdinov  kuruta aliwaua maafisa wawili na wanajeshi wenzake sita.

Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti kuwa mshukiwa huyo aliwalenga waathiriwa katika vichwa.

Tume maalumu inayoongozwa na Naibu Waziri wa Ulinzi, Andrey Kartapolov inaelekea eneo hilo ili kuchunguza mauaji hayo.

Kitengo hicho cha jeshi nambari 54160 kinahifadhi makombora.

Kina makombora ya Iskander ambayo yana uwezo wa kubeba vichwa vya kinyuklia.

Huduma za jeshi ni lazima nchini Urusi kwa wanaume wote walio kati ya umri wa miaka 18-27.

Wao huhudumu kwa miezi 12  na baadaye wanaweza kusaini kandarasi za kitaalam ili kuendelea kuhudumu katika jeshi.

Miaka ya 2000, makundi ya haki za kibinadamu yaliripoti ghasia na unyanyasaji kwa jina ”dedovshchina” dhidi ya makurutu wapya katika jeshi la Urusi.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni, Urusi inajivunia kuliimarisha jeshi lake na kuondoa unyanyasaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles