Wawili kortini mauaji ya kasisi

0
607

Nairobi,Kenya

MAHAKAMA imeamuru watu wawili wanaohusishwa na na mauaji ya kasisi wa Kanisa Katoliki. Michael Maingi Kyengo wasipewe dhamana hadi Novemba 6,mwaka huu.

Hakimu Mwandamizi, Hellen Onkwani aliagaza watuhimiwa Kavivya Mwangangi na Solomon Mwangangi wazuiliwe kituo cha polisi kwa muda wa siku nane ili uchunguzi zaidi kuhusu kifo cha kasisi huyo ukamilike.

“Badala ya usimulie kisa hicho hapa kortini, nitakuruhusu ufanye hivyo katika kituo cha polisi ukiandamana na watu wa familia yako na wakili ndipo urekodi polepole kilichojiri,” alisema Onkwani.

Mmoja wa maofisa wanaochunguza kesi hiyo, Julio Mutembei alijibu na kumweleza hakimu kuwa mshukiwa alitaka kutoboa siri jinsi kasisi alivyouawa.

“Naomba hii mahakama irekodi maungamo hayo ya mshukiwa huyu,” alisema Mutembei.

Hata hivyo, hakimu alikatiza huo ushahidi.

Mtuhumiwa mwingine, Michael Mutunga tayari anashikiliwa kwa muda wa siku 10 baada ya kufikishwa mahakamani.

Ijumaa iliyopita Mwangangi alisimulia korti jinsi mwendazake alivyofungwa mikono na miguu kabla kuuawa na maiti yake ikafukiwa kando ya mto katika Kaunti ya Machakos.

Alisema Padri Kyengo alikuwa amefungiwa ndani ya buti la gari.

Alimtaja Mutunga kama rafiki yake wa karibu ambaye alimwomba waandamane akamsaidie ‘kutoa sadaka.’

Alisema pia ni rafikiye ndiye aliyemwamuru kumfunga miguu na mikono marehemu.

“Msiniue tafadhali. Tafadhali usiniue,” Mwangagi alikumbuka jinsi kasisi huyo alimsihi Mutunga aliyekuwa amechukua simu ya Kasisi Kyengo.

Alieleza kuwa alimwamuru amtajie nambari ya siri ya kufungua simu na pesa alizokuwa nazo kwenye akaunti.

“Marehemu alimpa Mutunga nambari ya siri ya simu na akaunti za benki,” alisema Mwangagi.

Mtuhumiwa alisema Mutunga alitoa pesa kwa akaunti ya Kasisi Kyengo kisha akamlaza kifudifudi.

Mahakama ilielezwa utunga alichukua panga na kumuua Kasisi.

Mutembei aliieleza mahakama kuwa sampuli za marehemu zimepelekwa kuchunguzwa katika maabara ya Serikali.

Pia alisema nguo, gari, simu na kadi za benki zilichukuliwa na watuhumiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here