31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yadaiwa kumuua Baghdadi

WASHINGTON, Maekani

MAJESHI ya Marekani yamefanya oparesheni ya kumtafuta kiongozi mkimbizi wa wapiganaji wa Islamic State (IS), vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti.

Madai ya msako dhidi ya Abu Bakr al-Baghdadi hayajathibitishwa.

Lakini Ikulu ya White House, imesema Rais Donald Trump atatoa “taarifa kuu” siku ya Jumapili, haikutoa maelezo zaidi.

Rais Trump awali aliandika ujumbe katika Twitter yake akisema: “Kutu kikubwa sana kimefanyika!”

Kiongozi wa IS aliwahi kuripotiwa kimakosa kuwa amefarika siku zilizopita.

Maofisa ambao walinukuliwa na vyombo vya habari kuwa watu wasiojulikana walisema majeshi ya Marekani yanamsaka kiongozi wa kundi la Islamic State katika mkoa wa Idlib, kaskazini mashariki mwa Syria.

Kamanda wa vikosi vya Syria vinavyoongozwa na wapiganaji wa Kikurdi, Mazloum Abdi, siku ya Jumapili alisema kuwa oparesheni hiyo ya “kihistoria ilifaulu” kutokana na “kazi ya pamoja ya kiintelijensia” na Marekani.

Ofisa wa Marekani aliliambia Shirika la Habari la Reuters, kuwa oparesheni ilifanyika, lakini hakuweza kuthibitisha madai kama Baghdadi aliuawa.

White House haijathibitisha kuwa oparesheni hiyo ilifanyika, wala kukanusha matokeo yake.

Oparesheni hiyo ilifanywa na vikosi maalum baada ya kupokea “taarifa za uhakika”, Newsweek ilisema, ikiashiria vyanzo vya habari ambavyo haikutaja.

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Syrian Observatory, lenye makao makuu nchini Uingereza na ambalo limekuwa likichunguza kundi hilo, linasema mashabulio ya angani yaliwaua watu tisa katika kijiji kimoja mkoani Idlib ambako “makundi yaliyo na ufungamano na Islamic State ” yanamakao.

Habari zinasema, Rais Trump anatarajiwa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari baadae.

Hii sio mara ya kwanza kiongozi mkimbizi wa IS kuripotiwa kuuawa, lakini wikendi hii maofisa wa Marekaniwamekuwa wakizungumza kwa ujasiri kuhusu oparesheni inayomlenga.

Baghdadi  ambaye alikuwa akitumia jina la siri, badala ya jina lake halisi amekuwa kiongozi kiungo muhimu katika uongozi wa makundi ya kijihadi nchini Iraq na Syria tangu mwaka 2010.

Kabla ya hapo alizuiliwa katika Bucca iliyokuwa ikiendeshwa na Marekani kusini mwa Iraq, ambako alibuni ushirika na wanamgambo wa siku zijazo za IS.

Baada ya Syria kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na Serikali ya Iraq kuwabagua wa Waislamu wa dhehebu la Wasunni walio wachache.

Baghdadi aliunganisha wafuasi wachache wa waliosalia wa al-Qaeda kuwa kikosi cha mapigano ambacho kilifanikiwa kuuteka mji wa Raqqa huko Syria  mwaka 2013,kisha mji wa pili wa Mosul nchini Iraq mwaka uliofuata.

Kundi lake lililokuwa kikiendesha shughuli zake kwa ukatili mkubwa na ambalo lilidumu kwa miaka mitano liliwavutia maelfu ya wanamgambo wa kijihadiduniani.

Machi mwaka huu, lilipoteza sehemu ya mwisho eneo lake katika mji wa Baghuz nchini Syria.

IS imeapa kuendelea na mapigano “ya kuvizia” dhidi ya maadui wake.

Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi mkimbizi wa wapiganaji wa Islamic State (IS) na uongozi wake wa kidini amewekewa Dola za Marekani  milioni 25 na Serikali ya Marekani kwa mtu yeyote atakayempata.

Alizawa mwaka 1971 mjini Samarra, nchini Iraq, jina lake kamili ni Ibrahim Awad al-Badri.

Akiwa mfuasi mkuu wa dini ya Kiislamu tangu akiwa mdogo, baadaye alikuwa amefungwa katika kambi moja ya Marekani kwa jina Bucca mwaka 2004 kutokana na uvamizi wa Ufaransa na Marekani.

Akiwa katika kambi hiyo, aliweka ushirikiano mzuri na wafungwa wengine wakiwemo maafisa wa zamani wa ujasusi nchini Iraq.

Alijifunza mengi kuhusu jinsi anavyoweza kufanya operesheni zake kutoka kwa maafisa wa kijasusi wa aliyekuwa rais wa Iraq ,Sadaam Hussein.

Usalama wake ni wa hali ya juu ,kutokana na kiwango cha juu cha wasiwasi alionao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles