24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MUGABE ALIVYOMBADILIKIA TRUMP

NEW YORK, MAREKANI

RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amemwita mwenzake wa Marekani, Donald Trump, kuwa ni Goliati mkubwa ambaye anatishia kuzifuta nchi nyingine duniani, wakati akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini New York.

Mugabe amemshauri Trump kuzima tarumbeta lake mara moja, huku akiweka kumbukumbu kuwa aliwahi kutishiwa kuondolewa madarakani na Rais huyo mwenye utata aliyeingia madarakani mapema Januari 20, mwaka huu, akichukua nafasi ya Rais mstaafu, Barrack Obama.

Katika kipindi cha kampeni za kuwania urais wa Marekani, Trump alidokeza kuwa wapo viongozi wanatakiwa kung’olewa madarakani, akiwamo Robert Mugabe, huku akisisitiza kuwa, Bara la Afrika linapaswa kutawaliwa tena na wakoloni.

Akizungumza mkutanoni hapo, Mugabe alisema: “Wengine (sisi) tulijisikia fedheha sana, tulitishwa na hotuba ya Trump”.

Katika mkutano huo wa Rais wa Zimbabwe, Mugabe alimwambia Trump kuwa ni wakati wa “kupiga tarumbeta” lake kupigania amani. Hotuba ya Mugabe ilikuja baada ya Trump, aliyesimama mkutano hapo, kuzilaumu kwa nguvu nchi za Korea Kaskazini, Iran na Venezuela.

Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, alionekana kuchapa usingizi wakati Trump akitoa hotuba yake mapema wiki hii. Picha zinaonyesha kuwa, wakati Trump akitoa hotuba yake, yeye (Mugabe) alikuwa ameegesha kichwa chake kwenye kiti alichokalia pamoja na kufumba macho yake.

Aidha, inaonekana kuwa amesikiliza vya kutosha hotuba ya Trump ambayo imemkosoa, hali ambayo imechochea yeye kumwita rais huyo wa Marekani kuwa Goliati anayezungumzwa kwenye kitabu cha Wakristo cha Biblia. Goliati anaelezewa kwenye kitabu hicho kuwa alidhamiria kuiangamiza Israel, kabla ya kukumbana na baadaye kuuawa na Daudi.

“Huku ni kurudi kwa Goliati wa dhahabu, je, tupo tayari kumpokea Goliati huyu anayetishia ustawi wa nchi nyingine?  Naomba niseme hiki kwa Rais wa Marekani, Trump, tafadhali piga tarumbeta lako la kuthamini umoja, amani, ushirikiano, mshikamano, majadiliano, ambayo tunayo kwa kipindi chote,” alisema Mugabe.

Kiongozi huyo, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa sera za uvamizi za nchi za magharibi, ametumia hotuba yake kusema kuwa amelishinda dubwana la ubeberu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles