28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPENI YA LALA SALAMA UJERUMANI

MUNICH, UJERUMANI

WAGOMBEA wa vyama ndugu vya Christian Democratic Union (CDU) kinachoongozwa na Kansela Angela Merkel na Christian Social Union (CSU) vinatarajiwa kushinda katika uchaguzi mkuu wa hapa Ujerumani, utakaofanyika leo.

Iwapo Kansela Angela Merkel atachaguliwa kama kura za maoni zinavyotabiri, basi ataendelea kuongoza kwa muhula wa nne. Uchunguzi huo wa maoni wa hivi karibuni pia umeonyesha kuwa, chama hicho cha kihafidhina cha Kansela Merkel kitapoteza baadhi ya kura kama ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2013.

Chama cha Social Democratic (SPD) kinaweza kupata matokeo mabaya zaidi kwa mujibu wa kura hiyo ya maoni, lakini chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia cha AFD au maarufu kama chama mbadala kwa Ujerumani kinatarajiwa kuingia bungeni kwa mara ya kwanza kutokana na kuendelea kuungwa mkono na wapiga kura.

Katika harakati za kampeni za lala salama jana, Kansela Merkel aliwahutubia wafuasi wake mjini Munich, ambako pia alikabiliwa na kelele za wapinzani wake waliokuwa wanamtaka aachie madaraka.

Kansela Merkel atahitimisha kampeni zake kwa kurejea katika jimbo lake la nyumbani la Mecklenburg-Western Pomerania, wakati mgombea wa chama cha SPD, Martin Schulz, atahitimisha kampeni zake katika mji wa Aachen, ulio karibu na mji wake wa nyumbani wa Würselen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles