MOURINHO ANAVYOTESWA NA UWEPO WA GUARDIOLA EPL

0
30

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


 

USHINDANI unaoneshwa na kikosi cha Manchester City kinachoongozwa na  Pep Guardiola katika Ligi Kuu England msimu huu ni wazi kwamba unatoa changamoto kubwa kwa Jose Mourinho kutimiza lengo la United.

Manchester City  ambao wanaoongoza msimamo wa  ligi hiyo wakiwa na tofauti ya pointi tano na United wenye pointi 23 wanampa wakati mgumu Mourinho ambaye kwa sasa anasumbuliwa na presha za mashabiki wa timu hiyo ambao hawapendezwi kiwango cha timu yao.

Kutoakana na hali hiyo Mourinho, anatakiwa kuwa na hofu kuhusu kikosi cha Guardiola kutokana na kiwango chake msimu huu badala kujibishana na mashabiki wa United ambao hawana mpango wa kuisapoti timu yao kutokana na kiwango chake.

“Mfurahie soka” anasema Mourinho akiwataka mashabiki wa United wapunguze kuzungumzia timu yake mabaya kila muda na kujaribu kuwapa presha wachezaji wao.

Ilifikiriwa kwamba  sare dhidi ya Liverpool ingewavutia wachambuzi  na kuiona United bora kuliko Manchester City au kile kipigo  walichopata dhidi ya Huddersfield  kingeweza kuwaweka katika sinia moja na City ambao hawajafungwa tangu Agosti 21 mwaka huu.

United ambao walicheza na timu ya Chelsea jana ambayo Manchester City waliifunga  bao 1-0, mchezo huo utaongeza presha kwa Morinho na timu ya United kama hawatoshinda kwa sababu wataongeza pengo dhidi ya vinara wa ligi hiyo.

Katika mchzeo dhidi ya Tottenham walimaliza kwa aina yake.Walianza mechi katika kiwango  kibovu lakini walimaliza wakia mbele kwa ushindi wa bao 1-0, alilofunga Anthoy Martial akitokea benchi baada ya kupokea pasi iliyopigwa kwa kichwa na Romelu Lukaku.

“Ningependa mashabiki waeleze kwanini hawampi ushirikiano Lukaku kwa sababu anafanya kila awezalo kuisaidia timu, si sawa unapofunga bao  au kutofunga bao na mambo yakawa sawa sawa.

“Ukweli kuna vitendo sivielewi kama hawa ni Red Devil? Kuna wakati siwaelewi kwani washambuliaji wanafanya kazi yao vizuri, tulikuwa na wachezaji wawili dhidi ya walinzi watatu kama ambavyo tulifanya tulipokuwa kwenye michuano ya Europa, walifanya kazi ya ukabaji, lakini washambuliaji walitupa suluhisho kuepuka presha na kushinda.

“Lakini mashabiki wa klabu walilipia tiketi, hivyo wanaweza kufanya wanavyojisikia, wanaweza kuwazomea wachezaji ambao hawastahili kuzomewa na wanaweza kufanya pia kwa mchezaji ambaye anafanya kazi kama mnyama,”anasema Mourinho.

Mourinho alitaja neno mnyama  kama ambavyo mkongwe Sir Alf Ramsey alivyokuwa akimwelezea nyota wa Argentina, lakini ilikuwa zaidi ya Ramsey wakati Mourinho alipokuwa akielezea mchezo dhidi ya Tottenham.

Hata hivyo hakuna shabiki wa United aliyekuwa akilalamika kwamba  hajafurahia soka la vijana wa Mourinho kwa kumtoa Marcus Rashford na kuingia Lukaku.

Lakini Mourinho aliwataka mashabiki watambue kwamba kiwango cha Lukaku ni bora hasa baada ya kusababisha bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Tottenham.

Katika msimu wa kwanza  ambao  Mourinho aliweza  kunyakuwa mataji mawili, United  ilonekana  ingeweza  kuonesha ushindani mkubwa katika kwa ligi  mara ya kwanza tangu aondoke  Sir Alex Ferguson.

Mourinho aliweza kumshawishi Mkurugenzi wa  United, Ed Woodward  apewe  majukumu makubwa ndani ya klabu hiyo ikiwa pamoja na kusajili wachezaji ambao atawatumia  katika kupata ubingwa kwenye uongozi wake.

“Nafaham kuna njia tofauti katika kuchambua mambo, kama vile ubora wa baadhi ya klabu, kwa mfano mbinu wanazotumia pamoja na tabia za wachezaji.

“Kwa timu nyingine wakiwa na kiwango kinachofanana inakuwa hali tofauti na sifa nyingi kwao.kwa mfano Tottenham iliwafunga Liverpool mabao 4-1, Real Madrid mabao 3-1 lakini hawakupata bao walipocheza na sisi hivyo wachezaji wangu wanatakiwa kupata heshima yao katika jambo hili,”anasema Mourinho.

Rafiki wa karibu wa Mourinho, Jose Morais, ambaye  waliwahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Benfica, Inter, Real Madrid na Chelsea, mwezi uliopita aliuleza mtandao wa  MEN Sport kwamba Mreno huyo anaweza kukaa katika klabu misimu mitatu na kuondoka zake.

“Unaweza kuwa na furahaa kwa unafanya katika mazingira mazuri, unapata matokeo, na wakati huo huo, familia inakuwa na furaha, kila moja yupo vizuri,”anasema Morais.

Hata hivyo Mreno huyo anatakiwa kuhudhulia mahakamani nchini Hispania kujibu tuhuma zinazomkabili za ukwepaji wa kodi oauni milioni mbili mwaka 2011 na 2012, wakati akiwa kocha wa timu ya Real Madrid.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here