MOSCOW, URUSI
WAZIRI wa Habari wa Urusi, Dmitry Peskov amesema Rais Vladimir Putin wa hapa na Rais Donald Tump wa Marekani wataujadiliana kwa kina mgogoro wa Syria wakapokutana baadae mwezi huu.
Viongozi hao wawili wanatarajia kukutana mwezi huu wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Maendeleo Asia na Pasifiki (APEC) utakaofanyika nchini Vietnam.
Kwa sasa Rais Trump yupo katika ziara ndefu  ya kikazi katika nchi za Asia na Pasifiki.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Moscow, waziri alisema katika majadiliano ya marais hao kutakuwapo na ajenda nyingi lakini kubwa itakuwa ni kuhusu mgogoro wa Syria watakaoupangia muda zaidi ili kuupatia ufumbuzi.
Alisema kwa sasa kuna mafanikio mengi kuhusu kutatua mgogoro huo wa Syria,lakini kunahitajika ushirikiano mpya ili kuhakikisha amani inarejea katika maeneo ambayo yalikuwa yanakaliwa na magaidi wa kimataifa.