29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS ZAMBIA AWAONYA MAJAJI KUTOIGA KENYA

LUSAKA, ZAMBIA


RAIS Edgar Lungu amewaonya majaji nchini Zambia dhidi ya kumzuia kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2021, akisema aina ya utoaji maamuzi kama ya Kenya unaweza kuiingiza nchi katika machafuko.

Lungu anatarajia kuwania tena urais mwaka huo, lakini ana uwezekano wa kukabiliana na pingamizi za kisheria kutoka vyama vya upinzani, ambavyo vinasema katiba haimruhusu kugombea kwa sababu tayari ametumikia mihula miwili, ambayo ni ukomo unaoruhusiwa kisheria.

“Msiwe iga iga na kudhani ninyi ni mashujaa kwa kuiingiza nchi katika machafuko,” Lungu aliwaambia wafuasi wake katika tukio lililofanyika Solwezi, kaskazini magharibi mwa Zambia mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Nataka kufunga tukio hili kwa kusema wale watu wasiopenda amani na uhuru watadai ‘Rais Lungu anazitisha mahakama’ — kamwe sitishii mhimili wa mahakama.

“Nawaonya tu kwa sababu nina taarifa baadhi yenu mnataka kujitafutia sifa, tafadhari msituingize katika machafuko.”

Onyo hilo linakuja baada ya Kenya kujikuta katika mvutano wa miezi miwili uliotokana na uamuzi wa Mahakama ya Juu kufuta uchaguzi wa urais wa Agosti 8 baada ya kubaini kasro nyingi.

Iwapo Lungu atajisajiri rasmi kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2021, upinzani umepanga kwenda kupinga hilo katika Mahakama ya Katiba.

Katiba inasema rais anaweza kutumikia mihula miwili tu ya kila miaka mitano.

Lungu, ambaye mara ya kwanza alikuwa rais Januari 2015 baada ya kifo cha Michael Sata, alichaguiliwa tena kitatanishi mwaka 2016 lakini haifahamiki iwapo mihula hiyo inahesabika kuwa miwili nchini ya sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles