24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MATA: SOKA NI MCHEZO WA FARAJA

ADAM MKWEPU NA MITANDAO


KIUNGO wa timu ya Manchester United, Juan Mata anaamini kwamba mpango wa pamoja wa kusaidia mchezo wa soka kukua unaweza kuongeza faraja na kubadilisha maisha ya kila mtu duniani.

“Kwangu mpira wa miguu si ujuzi wala kipaji au idadi ya wachezaji unaowaongoza ila ni suala la kufanya uamuzi sahihi kila wakati unapokuwa na mpira ndani ya uwanja.

“Nimewaona wachezaji wanaofanya uamuzi kwa asilimia 100 wanapokuwa na mpira, kwa mfano, Andrea Iniesta na  Xavier “Xavi” Hernández, pia wachezaji wa Kingereza kama vile Paul Scholes, Frank Lampard na Steven Gerrard ambao wamefanya uamuzi sahihi mara nyingi kuliko makosa ndani ya uwanja.

“Unaweza kuwaona wachezaji wengi ambao wapo katika ubora wao wa  fiziki, wenye kasi na nguvu lakini hawawezi kufanya uamuzi sahihi wanapokuwa na mpira ndani ya uwanja,”anasema Mata.

Nyota huyo anaongeza kwamba jambo la muhimu kwake akiwa ndani ya uwanja ni kufanya kile ambacho anatakiwa kukifanya wakati huo.

“Kwa uhalisia unafaham kitu gani kizuri na kipi kibaya  hata kama unatakiwa kufikiri zaidi ugumu wa eneo la ulinzi na mfumo wake wakati unapokuwa uwanjani unakuwa huru kifikra.

Muhispania huyo ambaye amenyakuwa Kombe la Dunia, Europa ligi na ligi ya mabingwa ulaya  atachangia asilimia moja ya mshahara wake katika mpango wake mpya wa pamoja anaotaka kuzindua unaotambulika kama ‘Common Goal’ ambapo pesa hizo zinalengo la kusaidia watoto wenye vipaji katika soka duniani.

Lengo la Mata ni kuhakikisha anafikia nafasi ambayo kupitia mchango wake mpira wa miguu unatengeza fedha nyingi na kusaidia wengine.

“Si kuhusu mimi, wengine walitakiwa kuanza ila tayari nimeanza lakini natumaini  watachangia mpango huu, lengo ni kumfanya kila mtu afurahie mchezo huu na kusaidia wengine katika njia tofauti anayoweza kuifikia kwa urahisi.

“Njia nzuri ya kuanza ni kwa wachezaji wenyewe kwa kuwa tuna ushawishi mkubwa kwa wengine, tunazungumza kuhusu asilimia moja ya mshahara kwa kuwa tunahitaji kuwahamasisha wengine kuchangia,”anasema Mata.

Kama Mata atakuwa na hamasa katika kutoa kwa jamii kwa ajili ya maendeleo ya soka ni wazi kwamba dhamira yake katika anachokifanya ni jambo la fahari sana kwa sekta ya mchezo huo duniani.

Anakumbuka namna ambavyo alimpoteza babu yake miaka nane iliyopita hali iliyomfanya apambane ili kuboresha maisha yake.

“Ilikuwa siku mbaya katika maisha yangu,” anasema Mata baada ya kumpoteza baba yake na kuongeza kwamba: “Alikuwa ananiongoza kweda kwenye mazoezi  na kutazama mechi zote nilizotaka kutazama.

“Soka ndio ulikuwa mchezo anaoupenda na alikuwa mwenye furaha alipogundua nilikuwa naupenda pia.Ilikuwa na maana kubwa kutazama michuano ya Kombe la Dunia na ligi ya Mabingwa.

“Wakati nikicheza vizuri na kushinda mataji najihisi mwenye furaha sana, lakini najihisi pia mwenye furaha kwa familia yangu, nafaham wanavyopata taabu wakati mambo yakiwa hayaendi sawa kwangu,”anasema Mata.

Mata anasema kwamba familia yake wanakuwa katika wakati mgumu zaidi yake wakati akipita katika hali ngumu ndani na nje ya uwanja.

Mata alifunga bao muhimu katika mchezo dhidi ya Liverpool ambao Manchester United ilishinda mabao 2-1 katika uwanja wa Anfield mwaka 2015.

“Kabla babu yangu hajafa nakumbuka tulicheza dhidi ya Saint-Étienne na nilitoa pasi kwa Henrikh Mkhitaryan ambaye alifunga bao katika mchezo huo.

“Ilikuwa siku ya Jumanne na nilikuwa na matarajio ya kumuona tena baada ya fainali ya kombe la Capital One iliyotarajiwa kufanyika Jumapili, lakini alifariki Ijumaa, hivyo nililazimika kurudi Hispania na kurejea kwenye mchezo wa fainali.

“Tuliwahi kuzungumza mambo mengi baada ya mchezo dhidi ya Saint-Étienne. Afya yake ilikuwa dhaifu sana lakini aliniambia nilitoa pasi nzuri ya bao.Mazungumzo hayo nitayakumbuka katika maisha yangu yote, alikuwa mtu muhimu kwangu pia katika kazi yangu ya kucheza soka mchezo ambao unawafanya watu wengi wafurahi.

“Nimekuwa nikifikiria kuanzisha taasisi yangu ya kusaidia wengine.Lakini pia nikihamasishwa na dada yangu kwani ni mtu mwenye upendo na wengine, kwa sasa anaishi Iceland, anapenda kusafiri, nayapenda maisha yake,”anasema Mata.

Mata anasema kwamba familia yake inampa akili ya kufikiria soka katika njia tofauti ndio maana alikutana na  Jürgen Griesbeck.

“Amekuwa akijihusisha na soka kwa miaka 15 sasa alianzia nchini Colombia baada ya kifo cha Andrea Escobar ambaye aliuliwa baada ya kujifunga katika michuano ya kombe la dunia mwaka 1994.

“Baada ya kufanya mazungumzo kwa muda mrefu ndio tukaja na wazo la kuwasaidia wengine katika mchezo huu, tuliamua kuchangia asilimia moja katika maendeleo ya soka duniani,”anasema Mata.

Kiungo huyo anadai kwmaba anaelewa kwanini baadhi ya watu wanafikiri mchezo wa soka ni wakibinafsi.

“Si kazi rahisi kulifanya wazo kuwa katika uhalisia lakini Jurgen ana uzoefu katika jambo hilo na aliamini na kufaham kwamba ujumbe wa mchezo wenyewe una nguvu katika jamii.

“Siku si nyingi wachezaji wengine kama Mats Hummels, Giorgio Chiellini, Serge Gnabry, Dennis Aogo na wawili kutoka katika soka la wanawke nchini Marekani, Megan Rapinoe na Alex Morgan wataunga na mimi katika mpango huu,”anasema Mata.

Nahodha wa timu ya Sydney FC, Alex Brosque, pia amethibitisha kuunga na wenzake katika mpango huo wa pamoja katika maendeleo ya mchezo huo duniani.

Hata hivyo Mata hajazungumza na kocha wake Jose Mourinho kuhusu mpango huu wa pamoja: “Kuna wakati ni vigumu kufikiri jambo hili kutokana na maandalizi ya mechi hivyo inawezekana tutawasilina baada ya msimu kumalizika, jambo la msingi kuwasiliana na kila mmoja,”anasema Mata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles