23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

MASHABIKI SIMBA, YANGA USHAMBA HUU ZILIPENDWA

Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM


ILE ‘darby’ ya Kariakoo baina ya timu za Simba na Yanga inatarajia kuchezwa Jumamosi, ukiwa ni mchezo wa pili kwa timu hizo kukutana mwaka huu, baada ya ule wa Nago ya Jamii Agosti 23.

Baada ya miaka mingi kupita,  mechi baina ya timu hizo itachezwa kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam, huku Yanga wakiwa ndio wenyeji wa mchezo huo.

Kama ilivyo kawaida timu hizi zinapokutana kunakuwa na shamra shamra za hapa na pale kuanzia kwa mashabiki, viongozi, mabenchi ya ufundi na hata wachezaji, hiyo yote ni kuufanya mchezo huo kuonekana wa kipekee.

Ukiachana na masuala  yanayoashiria uwepo wa vitendo vya ushirikina vinavyofanywa na timu husika, mabaunsa wa klabu hizo pamoja na mashabiki, lakini yapo mambo yanayokera ambayo yamekuwa yakitokea ikiwa ni pamoja na vitendo vya vurugu uwanjani, hasa pale inapotokea timu moja kufungwa.

Mara nyingi vurugu hizi uanzishwa na mashabiki, ambao huonekana kutokubaliana na mamauzi yanayotolewa uwanjani au kutoridhika na matokeo yaliyopatikana.

Kuelekea mechi ya Jumamosi ni jambo zuri kwa mashabiki kufahamu kuwa mpira unamatokeo matatu, kufungwa, kushinda na kutoka sare, hivyo kitendo cha kutokubaliana na mambo hayo matatu ni sawa na ushamba uliopitwa na wakati.

Mpira ni mchezo wa amani na furaha, iweje kutokee vurugu kiasi cha kulazimisha vyombo vya usalama kutumia nguvu mfano wa mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na hata mbwa ili mradi tu kutuliza vurugu hizo.

Je vurugu zinazotokea na kuwalazimisha wanausalama kutumia nguvu, mashabiki mmeshajiuliza ni vitu vingapi vinaharibiwa na  mwisho timu zenu ndizo zinazolazimishwa kulipa gaharama.

Lakini pia je fedha hizo zinazotolewa kwajili ya kulipia vitu vilivyoharibiwa, mashabiki mmeshajiuliza zingetumika katika masuala mengine ya uendeshaji timu ingekuwaje?.

Ni wakati wa mashabiki kubadilika kwa kutambua mpira ni mchezo wa burudani na amani, wala sio ugomvi, vita au lugha za matusi mbazo zimekuwa zikitolewa kwenda kwa wachezaji na viongozi wa timu.

Ifahamike mechi ya Simba na Yanga inaonyeshwa sehemu kubwa Afrika kupitia runinga ya Azam FC, hivyo si jambo zuri wanaotazama kuona vurugu, badala ya burudani.

Matokeo yanayopatikana iwe Simba au Yanga imefungwa, kushinda au kutoka sare ni sehemu ya mchezo na sio iwe vita kwa mashabiki, wachezaji, mabenchi ya ufundi au viongozi wa timu, kwani huu ni ushamba unaotakiwa kuachwa mara moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles