MARCELO: NITAMALIZIA SOKA LANGU REAL MADRID

0
560MADRID, HISPANIA

BEKI wa pembeni wa klabu ya Real Madrid, Marcelo, amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo baada ya kuweka wazi kuwa, atamalizia soka lake ndani ya klabu hiyo.

Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus mara baada ya aliyekuwa mchezaji mwenzake Cristiano Ronaldo kujiunga wakati huu wa majira ya joto.

Marcelo amedai ataendelea kuwa ndani ya Santiago Bernabeu katika maisha yake ya soka hadi pale atakapo tangaza kustaafu soka lake. Mchezaji huyo raia wa nchini Brazil alijiunga na klabu hiyo mwaka 2007 akitokea Fluminense.

“Ni kitu kigumu kukizungumzia kwa sasa, lakini ukweli ni kwamba ninafurahia maisha ya hapa Real Madrid, naweza kusema kuwa, hapa ni nyumbani kwangu, nimebakisha miaka mingi ndani ya mkataba wangu.

“Nina furaha kuendelea kuwa hapa, hii ni klabu bora duniani, kila mara nimekuwa na lengo la kucheza kwenye kiwango kikubwa nikiwa na timu hii.

Ni vizuri kuzungumzia suala hilo ambalo limekuwa likienea kwenye mitandao ya kijamii, niweke wazi kuwa, nitaendelea kuwa hapa na ninataka kuwa hapa, nipo tayari kutumia uwezo wangu wote ili kuhakikisha timu inabaki kuwa bora duniani. Nitahakikisha ninazidi kuwa bora kila mwaka.

Ninafurahi kucheza kila mara na nitahakikisha ninaonesha ubora wangu ili kuwafanya mashabiki waendelee kuwa na furaha na timu yao. Mashabiki wasisikilize mambo ya kwenye mitandao, ukweli ninao mwenyewe kwamba, nitaendelea kuwa hapa kwa miaka mingi, najiona kama nina umri wa miaka 18, hivyo nitaendelea kuwa hapa hadi mwisho wa soka langu,” alisema Marcelo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here