ALEXIS SANCHEZ AACHANA MPENZI WAKE

0
889MANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United, Alexis Sanchez, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kuachana na mpenzi wake Mayte Rodrigruez.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, aliposti picha mbalimbali akiwa na mpenzi huyo pamoja na ujumbe wa kuuzunisha katika safari ya uhusiano wao.

“Ninakutakia kila la heri katika maisha yako mapya hapa duniani, ninayo furaha kukutana na wewe kwenye safari ya maisha yangu, kuna baadhi ya vitu tulivifanya pamoja, lakini tumefikia maamuzi ya kila mmoja kufanya vitu vyake vilivyopo kwenye ndoto zake.

“Baada ya tukio ili nataka kila mmoja aheshimu maamuzi haya kwa kuwa baada ya hapa kuna familia na watoto, hivyo heshima lazima iwepo,” aliandika Sanchez.

Ujumbe huo aliuandika huku akiambatanisha picha zao mbili ambazo zilipigwa wakati wa furaha yao na ujumbe huo uliwafikia zaidi ya wafuasi wake milioni tisa kwenye ukurasa huo wa Instagram.

Dalili za wawili hao kuachana zilianza kuonekana tangu Mei mwaka huu baada ya kila mmoja kufuta picha za mwenzake kwenye mitandao ya kijamii.

Mchezaji huyo aliongeza kwa kusema, kwenye uhusiano kuna mambo mengi ndani yake yanaendelea, lakini ni siri ya kila mmoja.

“Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na maneno mengi ambayo hayana ukweli ndani yake, ila kwa sasa ninamtakia kila la heri katika maisha yake mapya na wala hakuna ugomvi kati yetu, kikubwa ni kuheshimiana,” aliongeza.

Sanchez mwenye umri wa miaka 29, kwa sasa amedai anaangalia jinsi ya kurudisha kiwango chake kama ilivyo wakati anaitumikia klabu ya Arsenal, hivyo anajiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Watford ambao hawajapoteza mchezo wa Ligi Kuu.

Mchezo huo dhidi ya Watford utapigwa mara baada ya kumalizika kwa michezo ya kimataifa iliopo kwenye kalenda ya Fifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here