23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mambo matatu muhimu yatajwa miaka mitano ya M-Pawa

Mwandishi wetu

Benki ya CBA ikishirikiana na kampuni ya Vodacom imefanya droo yake ya nne ya kuadhimisha miaka mitano ya huduma ya MPawa yenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa wateja wake.

Droo hiyo ilifanyika Alhamisi Julai 4, kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam ambapo katika kuongelea kuhusu huduma  ya M-Pawa, Meneja Masoko wa benki hiyo Solomon Kawiche aligusia mambo matatu muhimu katika maadhimisho hayo.

M-Pawa inasherehekea miaka mtano, je ni mafanikio gani yameonekana tangu kuanzishwa kwa huduma hii?

Akijibu hoja hiyo Kawiche amesema M-Pawa imefanikiwa kutoa huduma ya kuhifadhi akiba kwa kiwango cha chini cha hadi shilingi 1, na kwamba hakuna benki nyingine nchini inayotoa huduma kama hiyo na kurahisisha huduma za kibenki bila ya kuwa na utaratibu mrefu wa kukamilisha miamala.

“Watumiaji wa M-Pawa hawana haja ya kutembelea matawi yetu na kupitia huduma hii, wateja wetu wanapata faida kupitia akiba zao. Akiba za wateja wa M-Pawa pia zipo kwenye usalama wa hali ya juu kwasababu hakuna makato au gharama zilizofichika,” alisema Kawiche.

Nini malengo ya baadae ya M-Pawa?

Akizungumzia hilo Kawiche amesema kuwa Ikiwa ni huduma ya kwanza ya kidigitali Tanzania, M-Pawa itaendelea kugusa masha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za kibenki na itaendelea kujidhatiti kwenye kuwajumuisha kifedha wateja wake.

“Kama benki, tuna malengo ya kuwekeza zaidi kwenye huduma hii kuhakikisha kuwa inaendana na maendeleo ya sasa ya kisayansi na Teknolojia na kuwezesha huduma hii kwenye application,” alisema Kawiche.

Nini maoni yako kwenye huduma za kifedha za kidigitali hususani M-Pawa?

Akijibu hoja hiyo M-Pawa inapatikana kupitia simu yoyote ya mkononi na kwamba ni huduma ya kibenki iliyorahisishwa kutumia mahali popote kwa gharama nafuu na humpatia mteja faida kupitia akiba anayoweka bila kuwa na gharama zilizofichwa.

“Hili linaupa upekee huduma hii ya M-Pawa na Mshindi mkubwa wa maadhimisho haya ataibuka na zawadi ya sh milioni  15  kwenye droo ya mwisho ya promosheni hii na kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii, wateja wanaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya benki ya CBA/Vodacom au kutembelea menyu ya M-Pawa kwa kubonyeza *150*00# kupitia mtandao wa Vodacom.

Promosheni hiyo inajumuisha droo za kila wiki zinazohusu kuwekeza na kukopa na M-Pawa huku ikitoa washindi zaidi ya 340 walioibuka na mara mbili ya akiba zao kuanzia kiwango cha Tsh 1000-200,000, simu janja na muda wa maongezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles