23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Amunike ndiyo basi tena Taifa Stars

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’  Emmanuel Amunike.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo Julai 8, imesema makubaliano hayo yamekuja baada ya pande zote mbili kufikia muafaka wa kusitisha mkataba wa kocha huyo raia wa Nigeria.

TFF itatangaza kocha wa muda atayekiongoza kikosi cha Taifa Stars katika mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

“Makocha wa muda watatangazwa baada ya kamati ya dharura ya kamati ya utendaji (Emergency Committee), itakapokutana Julai 11, mwaka huu,” imesema taarifa hiyo.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48, aliiongoza Stars katika michezo 10, alishinda miwili, sare mbili na kufungwa sita huku timu hiyo ikitolewa katika hatua ya makundi kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon), zinazoendelea nchini Misri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,097FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles