23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

Anna Potinus – Dar es Salaam

Rais John Magufuli amesema hana uhakika iwapo viongozi watakaokuja baadae wataweza kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu na kuhutaji viongozi kujitoa kwa moyo katika kufanikisha hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles