Baba Levo ahukumiwa miezi mitano jela

0
1240

Mwandishi Wetu

Mahakama ya Mwanzo ya Mwandiga mkoani Kigoma, imemhukumu Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Revocatus Kipando maarufu Baba Levo kwenda jela miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga askari wa Usalama Barabarani.

Baba Levo ambaye pia ni msanii wa bongo fleva, anadaiwa kumshambulia askari huyo akiwa kazini Julai 15, mwaka huu.

Hakimu wa Mahakama hiyo, Florence Ikorongo, ametoa hukumu hiyo leo Alhamisi Agosti Mosi, baada ya kusikiliza upande wa mshtakiwa akiwa na mashahidi wawili Mussa Lukomati na Karume Rashid.

Msanii huyo alimshambulia askari Msafiri Ponera, akiwa kazini eneo la Kwabwela baada ya kulazimisha kupita kwa pikipiki wakati askari huyo akiwawaruhusu watembea kwa miguu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here