24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli ashangaa waliomteka Mo kutofikishwa mahakamani

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amesema anashangaa ni kwa nini waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo), hawajafikishwa mahakamani hadi leo.

Rais amesema hayo leo Jumatatu Machi 4, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kuwaapisha mawaziri wawili na makamishna wa Jeshi la Polisi.

Akizungumza kuhusu Mo, Rais Magufuli amesema anashangaa kwa sababu wanaodaiwa kumteka walimtupa katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakaacha na silaha zao huku wakijaribu kuchoma gari moto lakini ilishindikana.

“Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania si wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo linaacha maswali….

“Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, baada ya tukio hilo tukamuona Mambosasa (Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa), anakunywa chai na aliyetekwa, baadaye tukaonyeshwa nyumba inayodaiwa kuwa alivyotekwa alihifadhiwa humo.

“Huyo mwenye nyumba alikuwa mtuhumiwa wa kwanza tulitegemea afikishwe mahakamani, kimya mpaka leo miezi imepita sasa hiyo inatoa maswali mengi ambayo majibu hayapo.

“Au ndiyo Mambosasa kama jina lake… kwa sababu Watanzania walitaka kujua huyo mwenye nyumba ni nani na angekuwa wa kwanza kukamatwa… Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa kimya,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles