25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Maalim Seif na Lowassa wakutana Dar

SEIF NA LOWASSANa Elias Msuya

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amekutana na aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chadema, Edward Lowassa, jijini Dar es Salaam jana na kusisitiza kuwa CUF haitarudia uchaguzi uliofutwa visiwani humo.Edward Lowassa

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam baada ya mkutano huo wa ndani, Maalim Seif alisema uchaguzi huo ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha binafsi.

“Msimamo wa CUF uko wazi, hatuoni sababu ya kuficha. Tangazo la mwenyekiti sisi tunaona si halali, kwa hivyo hatutashiriki…Tushiriki kwa sababu gani? Uchaguzi huu tulishashiriki, wenzetu hawataki, tuna uhakika gani kama huo mwingine watakubali?” alihoji Maalim Seif.

“Msimamo ni ule ule… hata ukisoma tangazo lile linasema mimi Salim Jecha, haikusema kama ni Serikali, limesema Jecha Salim.”

Alipoulizwa kuhusu mazungumzo yake na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Maalim Seif alikataa kuyaweka wazi akisema muda wake bado.

Hata alipoulizwa pia kuhusu mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete kuhusu mzozo huo, Maalim Seif alisema bado wakati wake wa kuyazungumza.

“Bado wakati wake, mtapata yote wakati ukifika,” alisema.

Naye Lowassa alipoulizwa kuhusu kamatakamata ya wasaidizi wake, aligoma kuzungumzia akimtaka msaidizi wake wa habari, Aboubakar Liongo aeleze.

Hata hivyo Liongo naye aliwataka waandishi wa habari kusubiri Jumapili, siku ambayo Lowassa atakutana na waandishi wa habari.

Awali Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, aliingia katika ofisi za Lowassa eneo la Mikocheni Viwandani majira ya saa 10 alasiri ambako walikuwa na kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa nzima.

Mbali ya Lowassa na Maalim Seif, wengine waliohudhuria kikao hicho cha ndani ni pamoja na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Twah Tasilima, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu na msaidizi wa siasa wa Lowassa, Matson Chizii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles