24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola aja na maagizo mapya kwa vyama vya siasa

Mwandishi wetu-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa onyo kwa vyama vya siasa nchini ambavyo vimetangaza kufanya mikutano ya hadhara kabla ya muda uliopangwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini.

Waziri Lugola ameyasema hayo wakati alipokuwa katika mahojiano maalum na chombo kimoja cha Habari jijini Dar es Salaam,  akisema jeshi la Polisi hivyo vyama vya siasa vilivyotangaza kuanza kufanya mikutano ya hadhara kabla ya muda vitashughulikia ipasavyo.

“Hii naomba ileweka na pia iwekwe akilini, mikutano ya hadhara bado haijaruhusiwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kosa kufanya mikutano ya hadhara kabla ya tarehe, jana kuna chama kimetangaza kuanza kufanya mikutano, sasa waendelee na mipango yao, alafu tuone nini kitawatokea.

“Kama wanataka kutikisa kiberiti cha Rais (John) Magufuli watakikuta kimejaa, wasithubutu kuichezea Serikali ya awamu hii, tupo imara na pia tutahakikisha tunalinda amani ya nchi kwa nguvu zote, amani hii tuliyonayo hatuwezi kuipoteza kamwe.

“Nimekabidhiwa lindo hili na Rais Magufuli ili niweze kulilinda ipasavyo, hivyo basi, wanasiasa wasibiri muda wa kuanza kampeni, sio kukurupa kufanya mikutano ya hadhara bila ya kufuata taratibu, hilo halikubaliki hata kidogo” alisema Lugola.

Pia Lugola, alisema kama kuna vituo vya polisi havitoi dhamana saa 24 kama alivyoelekeza, wananchi wampigie simu.

“Mwananchi yeyote atakayenyimwa dhamana, au atakaye onewa, akikisheni mnanipigia simu, na pia kuna njia nyingi za kutupa hapa Wizarani kupitia mitandao yetu ya kijamii, tovuti pamoja na makamanda mbalimbali walipo katika mikoa yote nchini,” alisema Lugola.

Aidha, Waziri Lugola amepiga marufuku tabia ya watu kuchukua sheria mkononi katika matukio yoyote yanayotokea nchini, alisema kumvamia mharifu na kumpiga ni kosa kisheria pamoja na matukio mengineyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles