31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

CCM waibuka kidedea uchaguzi Naibu Meya Dar

CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

MGOMBEA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Mtinika ameibuka mshindi katika nafasi ya unaibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, nafasi ambayo ataitumia kwa miezi nane kuanzia sasa.

Wagombea katika nafasi hiyo walikuwa ni Said na Ally Mohamed (CUF), ambaye alikuwa akitetea nafasi yake.

Said ambaye ni diwani wa Kata ya Kibondemaji Mbagala, alishinda nafasi hiyo kwa kura 16 kati ya 26 za wajumbe waliohudhuria baraza hilo.

Uchaguzi huo umeongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Issaya Mwita na Mkurugenzi wa Jiji, Spora Liana.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo, Mwita alisema kwakuwa akidi imetimia ni vema wajumbe wakashiriki ili kumpata kiongozi huyo ambaye nafasi yake ipo wazi.

Awali kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo, mgombea Patrick Assenga wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alijiondoa katika kinyang’anyiro hicho dakika chache kabla ya uchaguzi kuanza.

Assenga alisema ameamua kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho kwa sababu ana mheshimu mgombea mwenza Ally Mohamed wa (CUF).

Kabla ya kuanza kwa Uchaguzi, Mohamed aliyekuwa akitetea  nafasi yake alijiuzulu nafasi yake na kuwataka watumishi wa Jiji na Manispaa wamsamehe endapo aliwakwaza kwa namna yeyote katika kipindi chake cha uongozi.

Aliomba baraza hilo kumpa ridhaa ya kushika tena nafasi hiyo ili aweze kutekeleza aliyoyaanza.

Naye, Meya wa Ubungo, Boniphace Jackob, alisema amewaona baadhi ya wajumbe wamevaa majoho hawastahili kuwapo lakini Meya wa Jiji Mwita ameipitisha akidi wakati akifahamu kuna wasiofaa.

Akijibu hoja za uwapo wa mamluku, Mwita alisema wajumbe hao wawili wamepitishwa na menejimenti ya Jiji hivyo wapo kihalali.

Naye  Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee aliiomba baraza hilo limpe ridhaa ya kwenda kuhudhuria kesi Mahakamani na nafasi yake ya kupiga kura itapigwa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles