24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

KILA MISHE NI MZUKA MRADI MAPENE MFUKONI

Na RAMADHANI MASENGA

WANANGU niaje? Kila kitu frengwa ama magumashi tu? Acha kulalamika kiboya mwanangu. Haijawahi kutokea popote katika dunia raia wakaona mambo yako sawa.

Si unakumbuka bata walilokuwa wanakula Walibya kipindi cha utawala wa mzalendo Gaddaf? Sisi wa nje tulikuwa tunatamani kichizi lile laifu, ila wao ilikuwa vipi?

Walikuwa wanaona kama mwana anazingua hivi. Mbali na kila kitu kuwa free. Umeme free, maji free, elimu free na ukitaka kuvuta jiko, mwana alikuwa anatoa mchango pamoja na kukupa mjengo.

Ila yote hayo hayakuwa kitu mbele ya hawa binadamu waliokosa shukrani. Eti yakajazana rodi kudai demokrasia. Demokarasia ina maana gani kama hakuna kula, kuvaa vizuri wala elimu ya maana?

Wanangu mnajua ni kwanini nimetoa mfano huo? Nilitaka kuwaonesha namna binadamu wasivyo na shukrani kwa lolote. Na hata ufanye vipi lazima kuwapo watu wa kutoa lawama tu.

Sasa achana na kulalamika. Lawama hazifanyi mkate kuwa mkubwa. Pambana kila kona. Pambana bila kuchoka. Kama kuna mtu anakuambia hakuna mishe za kufanya siku hizi, muulize mwaka gani kulikuwa na mishe nyingi?

Kila awamu watu lazima walalamikie masuala ya mishe na chapaa. Sasa achana na lawama kama unataka kutoka. Amua kupambana mpaka mwisho.

Hakuna ujinga mkubwa kama kuamini huwezi kutoka. Sasa vipi uamini udwanzi huu wakati Mungu alikuleta duniani?

Unadhani Sir God alikuleta duniani kama nyongeza tu ya waliokuwepo? Shtuka mazee. Kila kitu kwa hii sayari ni mishe kama ukitumia vizuri bongo yako. Miaka kumi iliyopita nani aliamini kama chupa chakavu zinaweza kugeuka dili town? Shtuka wewe.

Wakati unalalamika kuwa hakuna mishe, hizo lawama zako watu wanazigeuza mtaji na kuingiza mabilioni ya pesa. Nikupe mifano?

Kwani unafikiri wanasiasa wanapiga vipi noti? Wao ni wajanja sana. Matatizo ya watu wao wanayageuza kuwa mitaji yao. Ndiyo maana katika mikutano yao ya kampeni wanasema watafanya hili na lile, kwa sababu na wewe umezoeshwa kulalama hovyo unadhani ni kweli.

Mwisho wa siku unawapigia kura, wanaingia mjengoni wewe unabaki maskani na milawama yako ya kindezi. Sisemi wote, wapo wanaofanya poa, lakini wengine dah! Hata kurudi twenty twenty hawana uhakika.

Acha kugeuzwa mtaji na wajanja wachache. Pambana. Hakuna mtu wala jini wa kuja kuleta unafuu wa laifu yako ikiwa wewe umekaa tu unapiga lawama badala ya kuchakarika. Mjanja michakato wewe.

Ujinga wa wana wengi ni kudhani kuwa mjanja huchagua kazi. Hakuna kuchagua kazi kama unataka mpunga. Unachagua kazi, je, unaweza kuchagua noti?

Nikikupa pesa iliyopatikana kwa mishe za kuuza mkaa na ile iliyopatikana kwa ubunge, utaacha ya mkaa na kukimbilia ya ubunge?

Buku kumi iliyopatikana kwa kuuza mkaa haina thamani kama elfu kumi iliyopatikana kwa kuwa mbunge? Zinduka wewe. Amka katafute mishe wewe, acha kulalalala.

Natimkia zangu kitaani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles