MIMBA KWA MASTAA FASHION TOWN!

0
1148

Na JOSEPH SHALUWA

NANI asiyejua kuwa mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobetto ni mjamzito? Ndiyo habari ya town. Listi ni ndefu.

Lakini katikati ya wiki hii, mrembo Wema Sepetu amempongeza msanii mwenzake wa filamu, Eshe Buheti kwa kupiga picha za staha akionyesha ujauzito wake.

Wema amempongeza Eshe kwa kupiga picha za heshima tofauti na baadhi ya wasanii wengine wa sasa wanaondekeza usasa kwa kupiga picha zenye ukakasi kulingana na mila na tamaduni zetu Waafrika na hasa hapa Tanzania.

Magazeti na majarida ya burudani huku mitandao ya kijamii ikizidi kusambaza zaidi, yameripoti wiki hii kuhusu mimba ya msanii wa filamu Kajala Masanja kutoka. Kajala mwenyewe amekaririwa akisema kuwa sababu ya ujauzito wake huo kuchoropoka ni matumizi ya dawa za maleria alizokunywa.

Kwa kauli yake mwenyewe, Kajala amekaririwa akisema anasikitika sana kupoteza mimba yake, maana mwanaye wa pekee Paula alikuwa akitamani sana kupata mdogo wake.

Tuachane na Kajala. Tukio ambalo halijapoa ni la msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga kupiga picha akionyesha ujauzito wake, lakini akiwa amevalia vinguo vya ndani huku akiwa amepaka mafuta mengi tumboni mwake.

Kitendo chake kilizua hisia za tafsiri tata miongoni mwa waungwana lakini mwenyewe alijitetea akisema kuwa, haoni maadili aliyovunja kwa vile hata mababu zetu walivaa kama alivyovaa.

Umesahau picha za msanii wa filamu, Aunt Ezekiel zilivyokiki Instagram wakati akiwa na ujauzito wa Cookie? Weka wote hao pembeni, lakini siku hizi kusikia fulani ana ujauzito ni jambo la kawaida kabisa.

Lakini ni kama kitu kigeni kidogo kwa jamii yetu, maana huko nyuma hapakuwa na utaratibu wa namna hii kabisa. Wasanii wengi walitaka kubaki vijana siku zote. Stori za mimba, kuzaa na kuolewa hazikuwa zenye kipaumbele sana kwao.

Unajua sababu? Uchambuzi unaendelea.

 

MASTAA HAWAPENDI KUZEEKA

Ilivyoeleka kwenye jamii yetu ni kwamba, suala la kubeba mimba na kuzaa ni kujizeesha. Wasanii wengi wa kike wa miaka ya nyuma hawakupenda kuhusishwa na mimba wala kuzaa.

Hali hiyo inaelezwa ilisababisha baadhi ya mastaa kudaiwa kuchoropoa mimba ili kulinda urembo wao na kuwaacha ‘wasichana’ siku zote.

Usanii ulionekana ni urembo zaidi kuliko kipaji kilichopo ndani. Hata hivyo, kwa wale wachache ambao waliamua kuzaa au kuolewa walifanya hivyo kwa siri kubwa.

Haikuwa rahisi hata kidogo kusikia kuwa msanii fulani eti ana mimba au amezaa. Utashangaa tu ghafla msanii fulani amepotea kwenye game  na baada ya miezi kadhaa utasikia msanii fulani amebahatika kupata mtoto.

Kuogopa huko kuzeeka ndipo kuliposababisha wasanii wengi wa kike kupitisha muda wa kuolewa kutokana na wanaume wengi kuwakimbia.

 

KUKUBALI MATOKEO

Wafuatiliaji wa maisha binafsi ya mastaa wanaeleza kuwa, wasanii wengi waliopo kwenye fani kuanzia miaka kumi iliyopita na kuendelea, umri wao umeshakwenda na hivyo kuona umuhimu wa kuingia kwenye ndoa.

Lakini kutokana na baadhi kukosa wanaume wakweli walio tayari kuingia kwenye ndoa, wameamua angalau wawe na watoto.

Sababu inayokaziwa zaidi inayosababisha mastaa hao waanike matumbo yao hadharani ni kuwaziba mdomo washakunaku wanaowatupia maneno kuwa hawana uwezo wa kuzaa tena.

 

NDOA BUTU

Ulimwenguni mwote mastaa wamekuwa wakisifika kwa kutodumu kwenye ndoa zao. Hili siyo la wanawake peke yao bali hata wanaume. Inaelezwa kuwa mastaa wanapooana ndipo tatizo huzidi na uwezekano wa kuachana huwa mkubwa zaidi.

Kutokana na ndoa hizo kuwa butu, imewafanya baadhi ya mastaa wa kike kuzikimbia na kujiweka mbali na rekodi mbaya, badala yake wameamua kukimbilia kuzaa ili kujiondoa kwenye listi ya wale wanaosemwa kuwa hawana uwezo wa kuzaa.

 

MIMBA HABARI YA MJINI

Kama ulikuwa na mawazo kuwa mastaa wanaogopa kuzaa sasa ujue kuwa siyo kwamba wanaogopa bali wapo tayari hata kuonyesha matumbo yao wakiwa wajawazito.

Suzan Michael, mfanyakazi wa salon moja ya kiume Kariakoo jijini Dar es Salaam, ameliambia Swaggaz la Mtanzania Jumamosi kuwa, wanawake huwa wapo tayari kufanya chochote kwa gharama yoyote ili kujiondoa kwenye lawama au kueleweka vibaya.

“Suala la kuonekana kuwa na mimba huwa wanaonekana sana… tatizo ni kwamba wanaonekana kwenye filamu, kwahiyo hata mtu akitupia picha Instagram akiwa mjamzito, bado ataonekana ni maigizo tu.

“Sasa ili kuondoa utata, ndiyo maana wasanii wengi wa kike wa siku hizi, wakiwa na ujauzito wanapiga picha wakiwa na matumbo wazi ili kuudhihirishia uma kuwa mimba iliyopo tumboni ni ya kweli na siyo filamu au scene ya wimbo mpya.

“Ujue sisi wanawake bana asikuambie mtu, hatupo tayari kabisa kukubali kudhalilishwa. Huwa tunakuwa tayari kutumia nguvu ya namna yoyote ile na hata gharama ikibidi ili kudeal na status zetu,” anasema Suzan.

 

TUWEKE KUMBUKUMBU SAWA..

Baadhi ya mastaa walioonyesha mimba zao ni pamoja na  Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ – mpenzi wa Diamond Plantinumz, Aunt Ezekiel – mpenzi wa Mose Iyobo na Chuchu Hans – mpenzi wa Vincent Kigosi – Ray.

Wengine ni hao niliowataja mwanzoni kabisa mwa makala haya. Wapo wengi lakini hawa wanaweza kueleza uhalisia wa mastaa wanaoonyesha wazi wamenasa ujauzito.

Siyo siri tena, ni jambo linalosubiriwa na wengi!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here