JUSTIN BIEBER, HAILEY NDOA YAKARIBIA

0
806

LOS ANGELES, MAREKANI


DALILI za ndoa ya staa wa muziki wa pop nchini Marekani, Justin Bieber na mwanamitindo, Hailey Baldwin, zimeanza kuonekana mara baada ya juzi mrembo huyo kuonekana akitoka nyumbani kwa mchungaji wa staa huyo.

Mapema mwezi huu kulikuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, Bieber na mrembo huyo wapo kwenye mipango ya kufunga ndoa mara baada ya kuvishana pete.

Bieber haumwambii kitu kwa mrembo huyo ambapo mapenzi yao yameonekana kuwa moto mara baada ya staa huyo aliyetamba na wimbo wa ‘Sorry’ kuachana na mpenzi wake Selena Gomez.

Mapenzi ya Bieber na Hailey, yanadaiwa kuanza tangu mwaka 2012, lakini yalikuwa ya siri sana, ila mwaka huu wameamua kuyaweka wazi na kudai wanataka kufunga ndoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here