FRED LOWASSA: NIACHIENI KALANGA NIMTIE ADABU

0
1652
Mwandishi Wetu, Monduli

Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Lowassa ameibukia katika mkutano wa kampeni za Ubunge uchaguzi Jimbo la Monduli na kuwataka aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo aliyejiuzulu, Julius Kalanga na Diwani wa Monduli Mjini, Isack Joseph maarufu Kadogoo, kukaa kimya kwani anawafahamu kuliko wanavyojifahamu.
Akizungumza kwenye mkutano huo wa kumnadi mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema, amelazimika kuwajibu vijana hao kutokana na kuendelea kumchafua Mzee Lowassa.
“Kama kuwatia adabu hawa vijana niachieni mimi, ntawatia adabu ninawafahamu vizuri sana.
“Niliwashika mkono kuwapeleka kwa mzee, sasa nawaomba tufanye siasa za kistaarabu hatuna tatizo na polisi, Mkuu wa Wilaya wala Rais John Magufuli na vingine vya dola,” amesema.
Aidha, mtoto huyo wa Lowassa ambaye awali  baadhi ya wanachama wa Chadema wilayani Monduli walijitokeza kumtaka agombee kupitia chama hicho, amesema wanamheshimu Rais, na wanaamini hauhitaji kuhama chama ili umheshimu Rais.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here