23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAKONTENA YA MAKONDA YAIBUA MAPYA DAR

Na Aziza Masoud-DAR ES SALAAM


MAKONTENA 20 yenye samani za shule yanayodaiwa kuwa ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  kwa mara ya pili jana yalishindikana kuuzwa kwa mnada baada ya wanunuaji kushindwa kufika bei.

Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart kwa idhini ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) iliyanadi makontena hayo jana katika ghala la Dar es Salaam Inland Container Deport (DICD) eneo la Bandari Kurasini.

Wiki iliyopita pia makontena hayo yalishindwa kupata wateja.

Sababu kubwa iliyotolewa jana na wateja ni kwamba makadirio ya bei yana walakini ukilinganisha na samani zilizoko kwenye makontena hayo.

Walisema samani hizo hazikupangwa kwa mpangilio na kwamba kama jambo hilo lingetekelezwa vizuri, zingetosha kwenye makontena matano tu na si 20.

Mnada wa makontena hayo ulianza saa 3:45 asubuhi.

Mbali na makontena hayo, pia kulikuwa na mengine yaliyokuwa na vifaa vingine kama matrekta, magari na vifaa vya kilimo.

Kati ya makontena 20 yanayodaiwa kuwa ya Makonda, kumi tu ndiyo yalikuwa katika eneo la mnada kwa sababu ya ufinyu wa nafasi.

Wanunuzi waliyakuta yakiwa yamefunguliwa ili waweze kukagua vitu vilivyomo.

Miongoni mwa vitu ambavyo vimeonekana katika makontena hayo kumi, ni pamoja na viti  vya kisasa vya kuzunguka ambavyo vinatumika ofisini, viti vya kisasa vya chuma vinavyotumika kukalia katika   hafla mbalimbali zikiwemo harusi, meza za ofisi, madroo ya kabati ambayo yanatumika kuhifadhia nyaraka ofisini na vingine.

MASHARTI YA MNADA

Kabla ya kuanza kwa mnada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono, Scolastika Kevela, alitoa masharti kwa washiriki ambapo pamoja na mambo mengine aliwatahadharisha waandishi wa habari nia yake ya kutaka usiri, hasa kwa wateja watakaofika bei ya makontena tofauti na ilivyokuwa ikifanyika katika minada ya siku za nyuma.

Kevela alisema wateja wa mnada …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles