23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

JPM MGENI RASMI BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA LEO

 

   Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 RAIS Dk. John Magufuli  anatarajiwa kuongo   za mkutano wa 11 wa Baraza Taifa la Biashara (TNBC) Ikulu, Dar es Salaam leo.

Taarifa iliyotolewa   Dar es Salaam jana na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,   Raymond Mbilinyi, ilisema maandalizi ya mkutano  huo yamekalimilika.

“Huu ni mkutano muhimu, sekta za umma na binafsi, unatoa fursa kwa pande mbili kujadiliana namna bora ya kujenga mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji zaidi nchini,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema mkutano huo  utakuwa wa pili kuuongozwa na Rais Dk. Magufuli kama  mwenyekiti wa  baraza tangu achaguliwe  mwaka 2015.

“Mkutano huu unafanyika wakati kukiwa na mafanikio makubwa ya viwanda zaidi 3,500 vilivyoanzishwa katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Maguful,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo  ilisema Serikali  imesimamia mabadiliko mbalimbali yaliyolenga kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuhamasisha ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda.

“TNBC ni jukwaa pekee la majadiliano ambalo hutoa fursa kwa sekta binafsi  Tanzania kujadiliana moja kwa moja na serikali kuhusu masuala ya kipaumbele kwa uchumi na ustawi wa maendeleo ya taifa,” alisisitiza.

Mabaraza ya Biashara ya Mikoa (RBCs) na ya wilaya (DBCs) chini ya wenyevikiti wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, yameweza kuhamasisha na kuibua fursa mbalimbali za  uchumi na maendeleo katika maeneo husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles