23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

MASHAHIDI 20 KUTUA KORTINI KESI YA MADABIDA, WENZAKE

NA KULWA MZEE,DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kuanza kusikiliza upya mashahidi 20 wa upande wa Jamhuri katika kesi ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya Ukimwi inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Ramadhani Madabida na wenzake watano.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Jamhuri kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo na kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali dhidi ya mashtaka yanayowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Mahakama hiyo imepanga kuanza kusikiliza ushahidi siku tatu mfululizo kuanzia Aprili 17, 18 na 19 mwaka huu.

Madabida na wenzake wanakabiliwa na mashtaka  ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya Ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara.

Washtakiwa wengine katikia kesi hiyo ni Seif Shamte ambaye ni Mkurugenzi  wa Uendeshaji,  Simon Msoffe Meneja Masoko na  Fatma Shango Mhasibu Msaidizi wote wafanyakazi wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd a na Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa.

Wakili wa Serikali Shadrack Kimaro, mshtakiwa Madabida, Shamte, Msoffe na Shango walikubali maelezo yao binafsi ikiwamo majina na nafasi zao za kazi.

Pia walikubali kuwa na usajili wa kuzalisha  dawa za ARV  TT-VIR 30 yenye viambata vya Stavudine 30 mg na Nevirapine 20mg na Lamivudine 150mg, ilisajiliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Walikubali kuwa muonekano wa plastiki za kuhifadhia vidonge uliosajiliwa ni wakuhifadhi vidonge 60 na kwamba MSD ilikuwa ni mteja mkubwa wa hiyo kampuni ya TPI.

Machi 17 mwaka 2009 MSD waliingia mkataba na TPI wa kusambaza hizo dawa za ARV na kwamba mkataba huo ulikuwa na thamani ya Sh 5, 236,845,200.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Joseph Mgaya alisaini mkataba huo kwa niaba ya MSD  na Kisah Lisha na Benjamin Kato ambao ni Mkurugenzi wa Masoko na Mkurugenzi Mtendaji wa TPI kwa pamoja waliingia hayo makubaliano kwa niaba ya TPI.

Washtakiwa hao waliendelea kukubali kuwa kwa kutumia mkataba huo, Machi 30, 2011 MSD waliamuru TPI kuwasambazia vikopo 19,300 vya dawa ya ARV kwa Dola za Marekani  155.172.

Walikubali  kwamba MSD iliagiza na agizo hilo lilitekelezwa na Joseph Mgaya kwa niaba ya MSD na Kisah Lisha kwa niaba ya TPI na kwamba mshtakiwa wa tatu alishuhudia utekelezaji wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles