25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Corona yavunja mechi ya Juventus na AC Milan

TURIN, ITALIA

MCHEZO wa mzunguko wa pili (marudiano) hatua ya nusu fainali ya Coppa Italia kati ya wenyeji Juventus dhidi ya AC Milan umehairishwa kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa Corona nchini HUMO.

Uamuzi huo umetolewa baada ya amri ya Waziri Mkuu kuainisha vizuizi vilivyowekwa katika hafla za michezo nchini kote hadi Machi 8, mwaka huu.

Mchezo huo wa marudiano ulipangwa kuchezwa jana bila mashabiki kutoka mikoa iliyoathiriwa zaidi, lakini badaye ulisogezwa mbele.

Hatua hiyo imetokana na mkutano ulihudhuriwa na Meya wa Turin Chiara Appendino, Claudio Paolomba, wawakilishi wa klabu na wizara za mitaa Jumanne.

Italia imeamua kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo tishio duniani kwa sasa ambao tayari umeshaua watu zaidi ya 3,000 kote ulimwenguni tangu ulivyolipuka nchini China mapema mwaka huu.

Taarifa ya Juventus ilisema: “Mchezo huo umeahirishwa kwa tarehe ambayo bado haijathibitishwa, kama ilivyotangazwa na Lega Serie A, baada ya kuchukua hatua kutoka kwa agizo la Jimbo la Turin n.14801 / 2019 / Area1 la 3 Machi 2020, ambalo ilitolewa baada ya mkutano wa leo [Jumanne] kumaliza. ”

Ripoti za vyombo vya habari sasa zinadai kuwa serikali ya Italia inazingatia kuahirisha hafla zote za michezo kwa mwezi mmoja ili kupunguza athari za ugonjwa huo.

Wakati huo huo, Wizara ya afya nchini Hispania imeliambia shirikisho la soka nchini humo kuamuru michezo ya Ligi YA Mabingwa Ulaya na ile ya  Europa Ligi  kufanyika bila ya mashabiki kufuatia hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa Corona.
.
Mechi hizo zitakazochezwa bila ya mashabiki ni dhidi ya klabu za Italia ambazo zinatoka nchini humo kunakodaiwa kuwa ugonjwa wa Corona tayari umeingia na umeshasababisha michezo kadhaa kuhairishwa.
.
Mechi ya marudiano ya klabu bingwa kati ya Valencia dhidi ya Atalanta itachezwa bila ya mashabiki.
.
Pia mechi kati ya Getafe dhidi ya Inter Milan ya michuano ya Europa Ligi  itachezwa bila ya uwepo wa mashabiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles