23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Klopp : kipigo cha Chelsea hakijanishtua

LONDON, ENGLAND

LICHA ya kikosi chake kupoteza michezo mitatu kati ya minne iliyopita, kocha wa Liverpool ,Jurgen Klopp amesisitiza kuwa hajashtushwa na fomu mbovu ya kikosi chake katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Chelsea,

Liverpool ilikumabana na kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa Kombe la FA uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Stamford Brigde, jijini London, hivyo kutolewa katika michuano hiyo.

Kichapo hicho kilikuwa cha tatu katika michezo minne ya hivi karibuni kwa kikkosi hicho kilichojiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Liverpool ilianza kukumbana na gundu baada ya kuchapwa Atletico Madrid bao 1-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiarudi na kuichapa West Ham mabao 3-2 katika ligi, kabla ya kufumuliwa mabao 3-0 na Watford katika ligi wikiendi iliyopita.

Kwa maana hiyo,kichapo hicho kimefuta matumaini ya Majogoo hao wa Anfield  kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja kama walivyowahi kufanya watani zao wa jadi, Manchester United mwaka 1999, ambapo walinyakua taji la Ligi Kuu England, FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Baada ya kupoteza mchezo huo, Klopp alisema fomu ya Liverpool haikumtia wasiwasi hasa baada ya kupoteza  mchezo wa tatu kati ya minne ya hivi karibuni.

“Tulipofungwa na Watford ilikuwa mbaya sana kwetu, lakini kichapo cha Chelsea hakikuwa kibaya sana.

“ Kwa kawaida haupati nafasi nyingi dhidi yetu, lakini inabidi tukubali kwenye michezo minne iliyopit tuliruhusu maboa mengi ya njia tofauti tofauti, sina shaka na kiwango chetu, siku zote tuna nafasi ya kurudia ubora wetu.

“Hatujawahi kufikiria utakuwa msimu rahisi, kipindi rahisi, mchezo rahisi usiku wa leo, hakuna chochote. ilikuwa ngumu kila wakati, usiku wa leo haukutosha na ndio tunapaswa kukubali.

“Kiwango chetu usiku wa leo ulikuwa tofauti kabisa na Watford,Watford alikuwa mbaya sana, usiku wa leo haikuwa mbaya, tulifanya mabadiliko saba na tulijua itakuwa ngumu ndio sababu tulifanya mabadiliko.

” Unahitaji kuharakishwa mara kwa mara ndio maana tulidhani tunabidi kufanya mabadiliko, sijali kuhusu kiwango cha leo,”alisema Mkufunzi huyo raia wa Ujerumani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles