25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Kagere, Bocco, Luis chini ya ulinzi

THERESIA GASPER – DAR ES SALAAM

MABEKI hatari wa Yanga, Juma Abdul na Andrew Vincent ‘Dante’, wamesema watahakikisha wanakuwa makini kuwadhibiti washambuliaji  hatari wa Simba, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili hii Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Miongoni mwa nyota wa kutumainiwa wa Simba wakati huu ni mshambuliaji Meddie Kagere, John Bocco na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone.

Timu hizo zitashuka dimbani zikiwa na kumbukumbu ya kutoka  sare ya mabao 2-2, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Januari 4 mwaka huu katika dimbani hapo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauto baada ya kumalizika kwa mchezo wao na Mbao juzi ambao Yanga ilishinda mabao 2-0, Abdul alisema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo ambao kwa kawaida uvuta hisia za watu wengi.

“Mechi hizi zinakuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia yake, kila mmoja amejiandaa kuhakikisha anaipatia timu yake matokeo mzuri ili iweze kutoka kifua mbele,” alisema.

Alisema Simba kuna wachezaji wazuri lakini na wao wapo vizuri na majukumu yake  kama beki ni kuwadhibiti washambuliaji wa timu pinzani wasilete madhara langoni mwao.

Kwa upande wa Dante alisema endapo atapata nafasi ya kucheza katika mchezo huo basi atahakikisha anafanya vizuri kwa kuhakikisha wapinzani wao hawapati bao.

“Mchezo huo mara nyingi unakuwa mgumu lakini  kwa upande wetu tunaendelea na maandalizi  ambayo tunaamini yatatufanya tupate matokeo mazuri mbele ya Simba,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles