Imechapishwa: Mon, Dec 18th, 2017

CHRIS BROWN AWALIZA WANAFUNZI, WALIMU

GEORGIA, MAREKANI


NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, mwishoni mwa wiki iliyopita aliwaliza wanafunzi na walimu katika shule ya Colombia Middle School, baada ya kutokea bila taarifa.

Msanii huyo ameamua kuumaliza mwaka kwa namna yake huku akidai kwamba anatoa zawadi ya sikukuu ya Krismasi kwa mashabiki zake.

Chris aliamua kutembelea shule hiyo na kutoa zawadi ya dola 50,000, ambazo ni sawa na shilingi 111,439,000 za Kitanzania. Baadhi ya walimu na wanafunzi walijikuta kutokwa na machozi ya furaha baada ya kumwona msanii huyo.

Mwalimu mmoja wa shule hiyo aliomba kupiga naye picha huku akiwa amemkumbatia, wakati huo baadhi ya wanafunzi walionekana kuimba nyimbo zake kwa furaha.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

CHRIS BROWN AWALIZA WANAFUNZI, WALIMU