29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

RAMSEY NOUAH AONYESHA PENGO ALILOLIACHA KANUMBA

Na JUMA3TATA RIPOTA


WIKI iliyopita tasnia ya burudani ilipokea ugeni wa mkongwe wa filamu kutoka nchini Nigeria, Ramsey Nouah, aliyekuja Tanzania kama mhamasishaji katika kongamano la vijana lililofanyika siku ya Alhamisi katika ukumbi wa Creative PFA, uliopo mkabara na chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Katika kongamano hilo lililolenga kuhamasisha vijana kujikwamua kimaisha na kutimiza ndoto zao liliwakutanisha wahamasisahaji wengine walikuwa ni Jokate Mwegelo na Idris Sultan ambapo vijana wengi wakiwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es salaam wanaochukua masomo ya mchepuo wa sanaa walijumuika ili kupata madini mapya.

Tukio lingine ambalo Ramsey Nouah, amelifanya na kuonyesha ni namna gani tasnia ya filamu ilivyopelekewa kimataifa na msanii kama Steven Kanumba, staa huyo alitembelea kaburi la msanii huyo maeneo ya Kinondoni, Dar es salaam.

Katika mazungumzo yake na vyombo vya habari, Ramsey Nouah alionyesha ni namna alivyokutana na Kanumba na wakazalisha filamu kali inayoitwa The Devils Kingdom ambayo walicheza pamoja miaka saba iliyopita.

“Steven, kwa mara ya mwisho tulizungumza sote tukiwa hai lakini leo nimesimama kando yako ukiwa umelala hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kwa kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili, najua huko uliko unaumia sana hususani ukizingatia ukweli kwamba tasnia ya filamu za kitanzania inakufa,” alisema Ramsey alipotembelea kaburi la Kanumba juzi.

Ramsey alionyesha kumkubali Kanumba kwa kuwa msanii mwenye uthubutu, msanii aliyependa kujifunza mambo mapya ndiyo maana alikuwa msaada mkubwa kwa tasnia ya filamu nchini kwenda kwenye anga la kimataifa.

Mkongwe huyo wa kiwanda cha filamu nchini Nigeria (Nollywood), alimwelezea Kanumba kama msanii aliyetumika kama daraja la kuwaunganisha wasanii wa nchi yake na Tanzania.

Daraja ambalo mpaka leo hii limeendelea kuwa alama ya mshikamano baina ya wasanii wa Nigeria na Tanzania lakini kabla hatujafaidi matunda ya uthubutu wa msanii huyo, Steven Kanumba akafariki dunia.

Baada ya kifo cha Kanumba, tasnia ya filamu imekuwa ikipitia kwenye wakati mgumu sokoni na wakati mwingine kupoteza mashabiki kutokana na wasanii wake kukosa uthubutu ambapo msanii huyo alikuwa nao enzi za uhai wake.

Ramsey Nouah ameonyesha ni namna gani Steven Kanumba ameacha pengo kwenye tasnia ya filamu barani, Afrika na kwa maneno yake hayo tunaweza kuona ni namna gani wasanii waliobaki wa filamu hapa nchini walivyo na kibarua kigumu cha kuziba pengo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles