24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

China yathibitisha kumshikilia bosi wa Interpol

BEIJING, CHINA

MAMLAKA za China zimethibitisha kumshikilia Mkuu wa Polisi wa Kimataifa (Interpol) aliyetoweka, Meng Hongwei.

Beijing imesema Meng anachunguzwa na Tume ya Kupambana na Rushwa nchini hapa kwa ukiukaji wa sheria.

Meng ambaye pia ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa umma China,  alitangazwa kutoweka baada ya kusafiri kutoka Lyon nchini Ufaransa yaliko makao makuu ya Interpol kwenda China Septemba 25.

Kutokana na tuhuma zinazomkabili, Meng amewasilisha barua ya kujiuzulu urais Interpol.

Familia yake haijawasiliana naye tangu aondoke makao hayo makuu ya Interpol.

Gazeti la South China Morning Post lilinukuu taarifa zilizosema Meng (64), alienda kuhojiwa China.

Haijulikani bado sababu ya kuchunguzwa na mamlaka za nidhamu wala mahali anaposhikiliwa.

Mapema wiki hii, mcheza filamu Fan Bingbin ambaye alitoweka nchini China, aliibuka akiomba radhi na kupigwa faini ya dola milioni 129 kwa kukwepa kulipa kodi na makosa mengine.

Meng alichaguliwa kuwa rais wa Interpol Novemba 2016 akiwa raia wa kwanza wa China kuchukua wadhifa huo, aliotarajia kuukamilisha mwaka 2020.

Meng pia bado ni mjumbe mwenye cheo cha juu katika Chama cha Kikomunisti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles