24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yatajwa mataifa yaliyo kikwazo mtangamano Afrika

ADDIS ABABA, ETHIOPIA

TANZANIA imetajwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa (AU) kuwa miongoni mwa mataifa ya Afrika yaliyo kikwazo cha mtangamano barani Afrika.

Ripoti hiyo ya hivi karibuni imebaini kuwa Waafrika wanaweza kutembelea asilimia 22 tu ya mataifa mengine ya bara hili bila visa.

Hili ni suala nyeti kwa baadhi ya mataifa kutokana na kadhia ya wenyeji kuwabagua wageni kwa kuhofia kupoteza nafasi zao za kazi.

Watunga sera kutoka Cape hadi Cairo wamekuwa na wakati mgumu kuwahamasisha watu umuhimu wa uhuru wa kutangamana wakisisitiza ni kiungo muhimu kwa ustawi wa uchumi.

Mfanyabiashara tajiri zaidi Afrika, Aliko Dangote, amesema anahitaji viza 38 za kusafiria katika mataifa tofauti barani humo akitumia pasipoti yake ya Nigeria.

Licha ya hayo, raia wengi wa mataifa ya bara la Ulaya huruhusiwa kuzuru mataifa ya Afrika bila hati hizo.

Mataifa ya Kiafrika yalitakiwa kufutilia mbali masharti ya visa kwa raia wote wa Afrika kufikia mwaka 2018.

Hii ilikuwa sehemu muhimu ya makubaliano na ushirikiano wa mataifa hayo iliyopitishwa na wanachama wote mwaka 2013.

Lakini hadi leo hii, Shelisheli ndilo taifa pekee barani Afrika lililoweka huru masharti ya usafiri kwa Waafrika wote na raia wa mataifa hayo.

Lakini maofisa wa uhamiaji nchini Burkina Faso huwatoza wasafiri kutoka Afrika ada dola 200 kupata visa wanapowasili nchini humo.

Kadhalika ripoti inasema Tanzania huwakamata na kuwarudisha makwao raia wa mataifa ya Afrika Mashariki wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria.

Tunisia pia imeripotiwa kuwanyima visa wasafiri wa Kiafrika waliokwama katika uwanja wa ndege baada ya ndege waliyokuwa wasafiri nayo kufuta safari.

Hii yote ni ishara ya wazi ya jinsi mataifa ya bara Afrika yasivyoaminiana.

Afrika Kusini imetajwa kuwa moja ya mataifa yanayoongoza kufungia mlango Waafrika huku ikifungua milango kwa mataifa mengine duniani.

Ni mataifa 15 pekee ya Afrika, ambayo raia wake wanaruhusiwa kuzuru Afrika Kusini bila visa huku ikiwapatia fursa raia wa mataifa 28 ya Ulaya kuingia nchini humo bila visa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles