24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yawatosa mawaziri waliobwagwa ubunge

 ccmPatricia Kimelemeta na Esther Mbussi, Dar es Salaam

LICHA ya Chama Cha Mpinduzi (CCM) kuamuru kurudiwa  uchaguzi katika baadhi ya majimbo yakiwamo  yaliyokuwa yanaongozwa na mawaziri wa Rais Jakaya Kikwete, hatimaye chama hicho kimewatosa rasmi.

Kutoswa kwa mawaziri hao kunatokana na kushindwa kwao kwenye kura za maoni za marudio ambako pia wana CCM wamebwaga katika mchakato huo na kusubiri hatima ya Kamati Kuu ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema baada ya kurudiwa  uchaguzi katika majimbo kadhaa hatimaye Kamati Kuu imefanya uteuzi wa mwisho huku ikiwaweka kando mawaziri hao.

Alisema   kikao kilichofanyika jana chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kimefanya uteuzi huo kutokana na matokeo ya kura za maoni.

Katika matokeo hayo ya kura za maoni, mawaziri  waliojikuta wakiangukia pua ni pamoja na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk. Titus Kamani   na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge.

Nape alisema katika kikao hicho cha CC pamoja na mambo mengine, kilikuwa na ajenda ya kupitisha majina ya wagombea katika majimbo yaliyorudia uchaguzi pamoja na Uchaguzi Mkuu

“Tumepitisha majina ya wagombea katika majimbo tisa  tuweze kusimamisha wagombea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu,” alisema Nape.

Aliwataja wagombea waliopitishwa katika majimbo hayo kuwa ni   aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry (Ukonga),  Edward Mwalongo (Njombe Kusini) na Venance Mwamoto (Kilolo).

Wengine ni Profesa Norman Sigala (Makete), Dk. Raphael Chegeni (Busega), Edwin Ngonyani (Namtumbo),  Martin Msuha (Chilonwa),  Joel Makanyanga (Mbinga Vijijini)   na Mohamed Mchengerwa (Rufiji).

Akizungumzia wanachama wa chama hicho wanaoendelea kulalamikia matokeo ya kura za maoni, Nape alisema wagombea hao walipaswa kuandika barua ya malalamiko yao kwa kamati kuu iweze kupitiwa na kutolewa uamuzi.

“Hakuna malalamiko yaliyowasilishwa kwenye kamati hii ambayo hayajafanyiwa kazi jambo ambalo lilisaidia baadhi ya majimbo kurudiwa   uchaguzi, hivyo basi wanachama wao wanapaswa kuacha malalamiko nje ya vikao.

“Kama wanaona chama hakijawatendea haki na kwamba CCM haiwezi kuwaletea maendeleo wanaweza kufanya uamuzi mgumu wa kujiunga na vyama vya upinzani ambako wanaamini wanaweza kutendewa haki.

“Ikiwa kuna mwanachama ambaye anaona haki anaweza kuipata akiwa upinzani na siyo CCM basi anaweza kwenda kutafuta hiyo haki, lakini kama CCM hatushughuliki na malalamiko ya nje bali tunashughulika na matatizo ya wananchi  na malalamiko ya ndani ya vikao,” alisema.

Kwa Lissu moto

Alisema katika jimbo la  Singida Mashariki ambalo linaongozwa na Mwansheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu   na jimbo la Karatu, yameonekana kukipasua kichwa chama hicho na hata kushindwa kufanya uteuzi wa majina kwa wagombea wake.

Alisema majimbo hayo ambayo ni kati ya majimbo 11 yaliyorudia uchaguzi wa kura za maoni  yameonekana kuwa na changamoto nyingi kuliko majimbo mengine tisa ambayo tayari yamekwisha kutolewa uamuzi na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM (Taifa) ya chama hicho jana.

Nape azushia jambo

Wakati huo huo, CCM kimekanusha taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya jamii kuwa Nape ameondolewa katika nafasi ya ukatibu uenezi na nafasi hiyo imechukuliwa na John Chiligati.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano, Daniel Chongolo,  alisema taarifa hizo si za kweli kwa sababu  kamati Kuu haijafanya uamuzi wowote wenye mlengo huo.

“Taarifa hizo zimeandaliwa kwa makusudi   kumchafua Nape,” alisema Chongolo.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles