24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

BUNGE LABARIKI MSAJILI KUFUTA VYAMA VYA SIASA

Fredy Azzah, Dodoma

Bunge limeiagiza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutosita kufuta chama chochote cha siasa kinachokiuka sheria, kanuni na taratibu za uendesheji wa vyama vya siasa nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa amesema hayo bungeni leo Jumatano aprili 4, wakati akitoa maoni ya kamati yake kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, mwaka 2018/19.

“Kamati inashauri na kusisitiza kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ihakikishe kunakuwa na usimamizi wa karibu kwa kufuatilia na kuchunguza mienendo inayoharibu sifa na vigezo vya vyama vya siasa nchini na kwamba Msajili asisite kufuta usajili wa chama chochote cha siasa kitakachokiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyama vya siasa,” inasema hotuba hiyo ya Kamati.

Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo imeishauri ofisi hiyo ifanye ufuatiliaji na na ukaguzi wa matumizi ya ruzuku kwa vyama vya siasa ili kuhakikisha kuwa matumizi ya ruzuku hizo yanazingatia madhumuni yaliyokusudiwa.

“Ikibainika ruzuku hizo zinatumika tofauti na madhumuni hayo, chama husika kisipewe ruzuku ili kutoa fundisho kwa vyama vyote kuzingatia matumizi stahiki ya fedha za wananchi,” alisema Mchengerwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles