22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

JENNA DEWAN, CHANNING WAACHANA

LOS ANGELES, MAREKANI


MASTAA wa filamu nchini Marekani, Channing Tatum na Jenna Dewan, wametangaza kuachana baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka tisa.

Wawili hao wenye umri wa miaka 37, wametumia akaunti zao za mitandao ya kijamii kusambaza habari hiyo ambayo imewashtua mashabiki wengi.

Hata hivyo, wameweka wazi kuwa wataendelea kuwa pamoja kama marafiki na watatoa huduma sahihi kwa mtoto wao wa kike Everly ambaye anatarajia kufikisha miaka mitano ifikapo Mei 31, mwaka huu.

Kwa mara ya mwisho wawili hao kuonekana wakiwa pamoja kabla ya kutangaza kuachana ilikuwa Novemba 6, mwaka jana kwenye tamasha la ‘LA premiere of War Dog’.

“Nataka dunia itambue kwamba kwa sasa sipo kwenye ndoa, hii ni taarifa mbaya lakini ndivyo ilivyo, nimefikia maamuzi ya kuachana na mume wangu baada ya kukaa pamoja kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka tisa, lakini tutaendelea kuwa pamoja kwa kumlea mtoto,” alisema Jenna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles