25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

BOT YARIDHIA KUUNGANISHA BENKI YA POSTA, TWIGA


Na JUSTIN DAMIAN-DAR ES SALAAM

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imetangaza rasmi kuridhia Benki ya Twiga Bancorp iliyokuwa chini ya uangalizi wake kuunganishwa na Benki ya Posta (TPB).

Hatua ya kuunganishwa kwa benki hizo imekuja baada ya BoT, kuiweka chini ya uangalizi maalumu kwa zaidi miaka miwili sasa.

Twiga Bancorp, iliwekwa chini ya uangalizi Oktoba 2016, kutokana na kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),  Dk. Benard Kibesse, alisema kuwa uamuzi wa kuziunganisha benki hizo unatokana na maombi yaliyowasilishwa kwao na mmiliki mkubwa wa benki hizo ambaye ni Serikali.

“Serikali ikiwa mmiliki mkubwa wa Twiga Bancorp imeamua kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa benki hiyo kwa kuiunganisha na TPB ambayo pia kwa sehemu kubwa, inamilikiwa na Serikali,” alisema Dk. Kibesse

“Kwa mamlaka iliyopewa BoT chini ya kifungu cha 30 (1) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2016, imeridhia kuunganishwa benki hizo mbili kuanzia Mei  17, 2018 (leo) na kwamba itakuwa ni benki moja itakayokuwa inaitwa TPB Benki PLC

“Muungao huu unamaanisha kuwa wateja, wafanyakazi, mali na madeni yote ya Twiga yatahamishiwa Benki ya TPB,” alisema.

Alipoulizwa kama mmiliki wa benki hizo mbili ana mpango wa kuongeza mtaji baada ya kuunganishwa, alisema Serikali ambaye ni mmiliki mkubwa haina mpango wowote wa kuongeza mtaji na kusisitiza kuwa TPB ina mtaji wa kutosha

Aliwataka wateja wa Twiga kuwa watulivu katika kipindi cha uunganishwaji na kuendelea kupata huduma za kibenki kwa utaratibu utakaowekwa na menejimenti ya TPB

Naibu gavana huyo,  alisema Serikali inapenda kuona mabenki nchini yakiungana na kuunda benki chache  zinazoweza kufanyakazi kwa ufanisi zaidi badala ya kuwa na utitiri wa benki zisizo na ufanisi.

Kwa upande wake, Meneja wa Bodi ya Bima ya Amana, Rosemary Tenga, alisema benki hiyo imeshalipa asilimia 60 ya madeni yanayotakiwa kulipwa kwa mujibu wa sheria kwa wateja waliokuwa wameweka amana katika benki ya Twiga

Alisema kwa sasa wanafanya ukaguzi wa hesabu ili kupata hali halisi ya mali na madeni, kazi ambayo itakamilika Juni mwaka huu

“Baada ya kupata hali halisi ya mali na madeni, tutauza mali na fedha zitakazopatikana zitalipa madeni na kama zitabaki zitagawiwa kwa wanahisa,” alisema

SAFARI YA BENKI YA TWIGA

Oktoba 28, 2016 Gavana  mstaafu wa  Benki Kuu ya Tanzania (BoT),  Profesa Benno Ndulu, alitangaza BoT kuchukua usimamizi wa Banki ya Twiga Bancorp kuanzia kutokana na upungufu wa mtaji wa benki hiyo.

Alisema BoT  ilichukua usimamizi wa Benki ya Twiga baada ya kubaini upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki.

Prof. Ndulu alisema shughuli zote za kibenki za benki hiyo zitasimamiwa na msimamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania  mpaka atakapopatikana mwekezaji wa kuendesha shughuli zote za kibenki hiyo.

JPM AGUSA JIPU

Novemba 4, 2016, Rais Dk. John Magufuli, aliwataka waandishi wa habari kufanya uchunguzi kwenye benki, ambako wanasiasa wamekopa mabilioni wa fedha ili waandike kwa kuwa mpaka sasa haijulikani kama wataweza kuzirudisha.

Akizungumza na wahariri katika mahojiano ya ana kwa ana Ikulu Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema wanasiasa wamekuwa wakichangia kufa kwa benki, kutokana na kukopa fedha nyingi  na kusababisha madeni makubwa.

“Benki zilikuwa zinakopesha wanasiasa wa Ukawa na CCM, lakini cha kushangaza hawarudishi fedha hizo na kuna benki zimefilisika, hivyo inabidi waanikwe hadharani bila kujali itikadi zao, ili kurejesha nidhamu katika ukopaji,” alisema Rais Magufuli bila kutaja benki hizo.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli, alikuja siku chache baada ya kufungwa kwa wiki moja kwa benki ya Twiga Bancorp, baada ya kuishiwa na mtaji uliopungua mpaka sifuri na kwenda hasi zaidi ya 20 na kusababisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuichukua ili kulinda amana za wateja, huku benki zingine zikilia hasara.

Alisema benki zipo 53 na zinawapa ahadi watendaji hao wa mashirika ya umma, ili kupata fedha hizo na kuzifanyia biashara kwa Serikali kwa kuikopesha kwa asilimia 15 hadi 16, lakini waliokuwa wanaumia ni wananchi wa chini, wanaolipa kodi inayotumika kulipa riba katika  benki hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles