Bieber, Hailey wapambana na ibada

0
1859

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya taarifa kuenea kwamba nyota wa muziki wa pop nchini Marekani, Justin Bieber na mpenzi wake Hailey Baldwin, wamefunga ndoa kimyakimya, wawili hao wamekuwa watu wa ibada kila wakati.

Taarifa za kufunga ndoa ya siri zilianza kuvuja tangu mwezi uliopita, lakini mrembo huyo alikanusha na kusema muda ukifika kila kitu watakiweka wazi, ila ukweli ni kwamba wamevishana pete ya uchumba.

Wawili hao juzi walionekana wakitoka katika Kanisa la Beverly Hills kwa ajili ya kumuomba Mungu ili mipango yao ikamilike.

Hata hivyo, Bieber mapema Agosti, alidai mwishoni mwa mwaka huu, atahakikisha anafunga ndoa na mrembo huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here