24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jiji la Dodoma laongoza ukusanyaji mapato Mbeya ikishika mkia

Bethsheba Wambura     



Jiji la Dodoma limeongoza katika ukusanyaji wa mapato kati ya majiji yote sita nchini ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 25 ambazo ni sawa na asilimia 130 ya lengo lake la kukusanya Sh bilioni 19 huku jiji la Mbeya likishika mkia kwa kukusanya Sh bilioni 7.8. ambazo ni sawa na asilimia 71 kati ya lengo la kukusanya Sh billioni 11.

Hayo yamesemwa na Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jaffo, jijini Dodoma leo Ijumaa Oktoba 5, wakati akisoma taarifa za matokeo ya ukusanywaji wa  mapato ya halmashauri za miji, mikoa na majiji zilizofanya vizuri na vibaya.

Jafo amezitaja halmashauri zilizofanya vizuri  ambapo Geita imeongoza kwa kukusanya kwa asilimia 218 na kuvuka lengo la kukusanya mapato kwa asilimia mia moja na  Mbinga ikifanya vibaya kwa kukusanya kwa asilimia 20 ikiwa haijafika hata robo ya lengo la kukusanya mapato kwa asilimia mia moja.

“Naagiza  wakuu wa mikoa na wilaya wa  halmashauri zilizofanya vibaya kuja ofisini kwangu na kutoa maelezo ya kina ni kwanini  zimefanya vibaya, haiwezekani kuwe na rasimali na vyanzo vya mapato na halmashauri ikusanye kwa asilimia 20, watendaji wake hawafanyi kazi zao ipasavyo.

“Haiwezekani Manispaa kama Ubungo yenye vyanzo vingi vya mapato na rasilimali ikusanye mapato kwa asilimia 42, inaonekana kuna wizi  watu wanakusanya fedha halafu wanaenda kutumia kwa matumizi binafsi badala ya kufanya kazi kwa maendeleo ya wananchi wanyonge,” amesema Jafo.

Aidha Jafo amewataka wakuu hao sio tu kufatilia makusanyo ya mapato ila wajue pia zinapokusanywa fedha hizo zinatumikaje na kama kuna watumishi wanajijua hawafanyi kazi zao ipasavyo kujiengua kabla hawajaenguliwa.

 

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Nashangaa sana Ikulu haikuwa imekanusha haya muda wote. Ni karibu wiki nzima tangu hiyo habari ya wake wawili kuanza kusambaa mtandaoni. Hivi kweli wahusika hawakujua kuhusu habari hizo wakazikanusha upesi?

  2. UKUSANYAJI WA MAPATO HAPA NCHINI
    Binafsi naamini kwamba tatizo la ukusanyaji wa mapato kiduchu linatokana na sababu kadhaa na sio tu usimamizi mbovu.
    Naamini kwamba MFUMO wa ukusanyaji mapato unatakiwa UBADILISHWE KABISA. Huu mfumo wa sasa unaotegemea kudai kodi kutokana na mahesabu yanayotengenezwa na mlipakodi kwetu sisi Tanzania HAUTUFAI.

    Nasema hivyo kwa kuwa a) Ni wafanyabiashara wengi sana hawajui au kwa makusudi wanaacha kukusanya kumbukumbu za mauzo na manunuzi. Kwa hiyo, mahesabu yao hayawezi kuwa sahihi. Hivyo inabidi rushwa itolewe ili kibali cha kodi (tax assessment) yenye kodi ndogo kitolewe.
    b) Wapo wafanyabiashara wengi tu ambao kwa nia ya kukwepa kodi hawachukui malipo ya fedha bali ya bidhaa au wakichukua fedha haziingizwi kwenye vitabu. Kwa mfano kama mimi Mr. A nauza nguo za jumla na nahitaji kujengewa nyumba na Mr B ambaye ni mkandarasi na sote wawili tunafahamiana na Mr C ambaye ana biashara ya nguo rejareja na pia ana biashara ingine ya kuuza vifaa vya ujenzi, tunaweza kukubaliana wote watatu tukafanya “biashara kubwa” ya milioni mia kadhaa bila fedha kuzunguka. Mimi nitampa Mr Mr C nguo zenye thamani inayolingana na vifaa vya ujenzi anavyohitaji Mr B. Fedha nitakazotoa ni za kulipa tu ufundi na vibarua.

    Njia moja ya kuweza kuhakikisha kwamba kila mwananchi analipa kodi bila kusumbuliwa na maofisa kodi lakini analipa kodi stahiki ni njia rahisi tu. Ni kuhakikisha tu kwamba mali zinazonunuliwa na kila mwenye kiwanda zinajulikana. Unaweza kuwekwa mfumo wa kuhakiki mali za huyo mfanyabiashara na kuzilinganisha na kumbukumbu za kununulia. Zikishajulikana, kiasi sahihi cha kodi ambacho huyo mfanyabiashara anaweza kulipa kinaweza kukadiriwa. Baada ya hapo, huyo mfanyabiashara awe anapeleka kodi yake TRA kama vile mtu anayerejesha mkopo, kidogo kidogo. Kwa nini tulazimike kumfanya mfanyabiashara alipe awamu za kodi kila robo mwaka na sio kila mwezi na kila anapopata uwezo wa kulipa?

    Tukitumbua viongozi wa wilaya ambayo haijakusanya vizuri bado hatutaweza kuwafanya walipa kodi walipe kodi stahiki kama hatujabadilisha mfumo wa kodi. Na vyanzo vya kodi vinaweza vikabadilika mwaka kwa mwaka. Inawezekana Dodoma imekusanya kodi kubwa sana kwa vile viwanja vingi vimetolewa baada ya Dodoma kuwa makao makuu na chanzo hicho kikaongeza kiasi cha makusanyo. Kama kila mfanyabiashara angekuwa analipa sehemu ya kodi yake kila mwezi kama nilivyopendekeza hapo juu, nadhani tungekuwa tunakusanya kodi nyingi. Kazi za maofisa kodi iwe ni kupita kwenye kila biashara na kucheki kama kodi ya mwezi uliotangulia imelipwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles