24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

AJIB, MANYIKA WAREJESHWA STARS

Na ABDUL MKEYENGE, DAR ES SALAAM

WACHEZAJI Ibrahim Ajib na Manyika Peter ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) na Kocha Salum Mayanga kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi ‘The Flame’.

Mayanga amewaita nyota hao kwa ajili ya mchezo huo ulio ndani ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), utakaofanyika Oktoba 7, kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Akitangaza majina ya wachezaji hao pamoja na wachezaji wengine 20 mbele ya waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam, katika hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kocha huyo amewaita nyota watano wanaocheza nje.

Kikosi hicho kinachotarajiwa kuingia kambini wiki ijayo kwenye Hoteli ya Sea Scape, iliyoko jijini hapa, kinaundwa na makipa Aishi Manula (Simba), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Manyika (Singida United).

Walinzi Gadiel Michael (Yanga), Boniphace Maganga (Mbao), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde na Erasto Nyoni (Simba) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).

Viungo ni Himid Mao (Azam), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba) na Raphael Daud (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shizza Kichuya (Simba), Abdul Hilal (Tusker/Kenya), Ajib (Yanga) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Mbaraka Yussuph (Azam FC). Benchi hilo la Mayanga linaundwa na Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Richard Yomba (Daktari wa timu), Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

Nyota waliokuwapo kwenye mchezo wa mwisho wa Stars waliocheza dhidi ya Botswana na kushinda mabao 2-0 na hawajaitwa katika kikosi hiki ni Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (CD Tenerife/Hispania), Said Ndemla (Simba) na Mwadini Ally (Azam).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles